Sunday, June 22, 2014


Xabi Alonso, Kiungo wa Real Madrid, ametangaza kustaafu kuichezea Nchi yake Spain.
Alonso, Miaka 32, amekuwa mmoja wa kiini cha mafaniko ya Spain iliyotwaa EURO 2008 na EURO 2012 pamoja na Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwaka 2010.
Juzi Alonso aliichezea Spain Mechi yake ya 112 ilipofungwa 2-0 na Chile kwenye Mechi Kundi B na kutupwa nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.

Kwenye Mechi hiyo, Alonso alibadilishwa wakati wa Mapumziko baada kupwaya na kupokonywa Mpira uliozaa Bao la Kwanza la Chile.
Lakini Alonso ndie Mchezaji pekee aliewafungia Spain Bao pekee kwenye Mashindano haya huko Brazil alipofunga kwa Penati kwenye Mechi ya Kwanza ya Kundi B waliponyukwa Bao 5-1 na Netherlands.

Mara baada ya Spain kutupwa nje ya Fainali ya Kombe la Dunia, Alonso alisema: “Vitu vinabadilika. Zama zinaisha kwa kufungwa…na hiki kilikuwa kipigo kichungu. Hatukutegemea lakini ndio mchezo. Hivi vitu vinatokea. Hatukutegemea lakini ni lazima tuyakabili majonzi yetu vile vile kama tunavyofurahia, kama Wanaume.”

Aliongeza: “Tumecheza dhidi ya Timu zilizojitayarisha vyema na sasa tunarudi nyumbani. Inauma lakini huu ndio mpira. Kama nilivyosema, tulijua namna ya kushinda, sasa inabidi tujue namna ya kushindwa!”

Mbali ya Alonso kutangaza kustaafu pia kuna wasiwasi kuwa Kiungo Xavi na Kipa Iker Casillas, ambao wote wamecheza ovyo huko Brazil, wanaweza kufuata nyayo zake.
Zipo habari kuwa Kocha wa Spain, Vicente del Bosque, hasa kwa vile Shirikisho la Soccer la Spain, RFEF, linaunga mkono aendelee na kazi yake.


KUHUSU REKODI YA XABI ALONSO
BORN: Tolosa, Spain, November 25, 1981

1999-2000: Real Sociedad B (39 apps, 2 gls)
1999-2004: Real Sociedad (114 apps, 9 gls)
2000-2001: Eibar (loan) (14 apps, 0 gls)
2004-2009: Liverpool (143 apps, 15 gls)
2009-NOW: Real Madrid (158 apps, 4 gls)



2003-NOW: Spain (112 caps, 16 gls)
CLUB HONOURS:

LIVERPOOL - FA Cup (2006), FA Community Shield (2006), Champions League (2005), UEFA Super Cup (2005)
REAL MADRID - La Liga (2012), Copa del Rey (2011, 2014), Supercopa de Espana (2012), Champions League (2014)
SPAIN - World Cup (2010), European Championship (2008, 2012)

WORLD CUP 2014: NIGERIA 1 vs BOSNIA-HERZEGOVINA 0, PETER ODEMWINGIE AWAPATIA USHINDI NIGERIA..

1-0, Peter Odemwingie kushoto akishangilia bao lake lililotosha kuwapatia alama 3 muhimu na kuwawezesha kuwa na jumala ya pointi 4 na wako nafasi ya pili kwenye kundi lao na mtanange ujao kwa Nigeria ni jumatano tarehe 25 saa moja kamili.Peter Odemwingie dakika ya 29 aliifungia bao timu yake baada ya kazi nzuri ya Emenike kwa kuwakacha mabeki wa Bosnia na kumpa pasi Odemwingie na kufunga bao huku wachezaji wa Bosnia wakishindwa kuamini bao hilo.
Mchezaji wa Bosnia midfielder Izet Hajrovic akipitwa na mchezaji wa Nigeria difenda Juwon Oshaniwa na kwenda eneo la hatari la kipa na kugawa pasi kwa Peter Odemwingie

Friday, June 20, 2014


Warembo wanaowania taji la mkoa wa Tanga, Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakijiaandaa kufanya usafi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ikiwa ni moja ya kampeni ya kuendelea kulifanya jiji hilo liwe safi muda wote. Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakitupa takataka katika gari maalum la kubeba taka. Mshindi wa kwanza katika shindano hilo atapata zawadi ya gari dogo aina ya Toyota Vitz. Zoezi la usafi limepamba moto na kuliacha eneo hilo safi kabisa. Mgeni rasmi katika shindano hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Chiki Gallawa.


Suarez baada ya kuimaliza England kwa bao 2-1.Luis Suarez akishangilia bao lake baada ya kuifungia Uruguay kwa bao la kichwa katika kipindi cha kwanza dakika ya 39 baada ya kupata ushirikiano mzuri  kutoka kwa Edinson Cavani. Dakika ya 75 Wayne Roone ndie aliyeisawazishia bao England baada ya mabeki wa Uruguay kujisahau na hatimaye Glen Johnson kumsogezea mpira Roone na kufunga bao hilo. Bao hilo la Rooney halikuweza kudumu kwani dakika ya 85 Luis Suarez aliwachoma bao jingine England na kuwapatia Ushindi Uruguay na mpira kumalizika wakiwa wababe kwa bao hizo mbili zilizofungwa na mchezaji mmoja Suarez kwa matokeo ya 2-1.Patashika..Kipindi cha kwanza
VIKOSI:
Uruguay:
Muslera, Gimenez, Godin, Caceres, Pereira, Lodeiro, Gonzalez, Arevalo Rios, Rodriguez, Cavani, Suarez.
Subs: Munoz, Fucile, Gargano, Hernandez, Forlan, Stuani, Perez, Ramirez, Coates, Maxi Pereira, Silva.

England: Hart, Baines, Cahill, Jagielka, Johnson, Gerrard, Henderson, Sterling, Rooney, Welbeck, Sturridge.
Subs: Foster, Wilshere, Lampard, Smalling, Jones, Milner, Lambert, Lallana,
Barkley, Shaw, Forster.
Referee: Carlos Velasco Carballo (Spain)
Wayne Rooney ndani kucheza nafasi ipi usiku huu..kati au pembeni?

Luis Suarez baada ya kuukosa mtanange wa kwanza leo hii  ndani  Uruguay ikiumana na England usiku huu

Thursday, June 19, 2014

Itakuwa Mechi ya ‘Kufa na Kupona’ maana yeyote atakaefungwa atakuwa na nafasi finyu mno kutinga Raundi ya Pili ya Fainali za Kombe la Dunia baada ya zote, England na Uruguay, kufungwa Mechi zao za Kwanza za Kundi D.
England walichapwa 2-1 na Italy na Uruguay kudundwa 3-1 na Costa Rica.
England warm up during an England training session ahead of the 2014 FIFA World Cup Brazil match against Uruguay at Arena de Sao PauloWachezaji wa England wakijifua Sao Paulo masaa 24 kabla ya kukutana uso kwa uso na UruguayMeneja wa England HodgsonEngland pose for a team photo Straika wa Uruguay Luis Suarez yuko fiti baada ya kupona maumivu ya Goti lakini watamkosa Nahodha wao Diego Lugano ambae ameumia Gotu na pia Maxi Pereira mwenye Kadi Nyekundu.
Mchezaji pekee wa England mwenye hatihati kucheza ni Alex Oxlade-Chamberlain ambae aliumia Goti lakini amerejea tena Mazoezini.
Hii ni Mechi ambayo England na Uruguay lazima zishinde.
Akiongelea Mechi hii, Luis Suarez, ambae ndie alietwaa Tuzo za Mchezaji Bora huko England, amesema: “Nawajua Wachezaji wote wa England. Ama ni wenzangu Klabuni au ni Wapinzani kwenye Mechi. 

Wana kasoro kwenye Difensi ambazo tunaweza kuzitumia.”
Lakini Straika wa England, Daniel Sturridge, anaecheza Klabu ya Liverpool pamoja na Suarez, amechochea moto kwa kutamka: “Nitafanya kila niwezalo tushinde mradi iwe ndani ya Sheria lakini sitajiangusha na wala sitashika Mpira Golini kwa sababu si hulka yangu!”
Maneno hayo moja kwa moja yamemlenga Suarez kwa matukio yake Siku za nyuma.



Uso kwa Uso
-Kwenye Fainali za Kombe la Dunia, England na Uruguay zimekutana mara mbili kwa Uruguay kushinda 4-2 Mwaka 1954 na kutoka 0-0 Mwaka 1966.
-Mara ya mwisho kukutana ni Machi 2006 Uwanjani Anfield kwenye Mechi ya Kirafiki na England kushinda 2-1 kwa Bao za Peter Crouch na Joe Cole.

Wednesday, June 18, 2014


Ligi kuu England itaanza Agosti 16 na leo hii Ratiba ya Msimu mpya wa 2014/15 imetangazwa.
Mabingwa Manchester City wataanza Ugenini na Newcastle wakati Meneja mpya wa Manchester United, Louis van Gaal, atakuwa Nyumbani Old Trafford kucheza na Swansea City.
Arsenal wataanza Nyumbani kucheza na Crystal Palace na Chelsea wako Ugenini kuivaa Timu mpya iliyopanda Daraja Burnley.
Siku hiyo ya Ufunguzi, Anfield itashuhudia Timu yao Liverpool ikicheza na Southampton.
Bila shaka pambano la mwanzo la mvuto mkubwa ni lile litakalochezwa Etihad Agosti 23 kati ya Man City na Liverpool waliomaliza Nafasi ya Pili Msimu uliopita.
Hapo Agosti 9, Uwanjani Wembley, kutakuwa na pambano la Kufungua Pazia Msimu kugombea Ngao ya Jamii kati ya Man City, ambao ni Mabingwa, na Arsenal, Mabingwa wa FA CUP.
Man United na Meneja wao mpya kutoka Holland,  Louis van Gaal kuiongoza  Manchester United wakiwa Nyumbani Old Trafford.

Mabinwa Manchester City wana kazi nzito kuanzia Ugenini na Newcastle

Joe Hart akishangilia na wenzake msimu uliomalizika

Monday, June 16, 2014


Bao la pili kwa Argentina lilifungwa na Staa Lionel Messi alipowachambua mabeki na kuachia shuti kali kipindi cha pili dakika ya 65, Akipewa pasi safi na Gonzalo Higuaín. 
Mchezaji aliyeingia kipindi cha pili akitokea benchi Vedad Ibisevic aliwafunga Argentina bao la kizembe katika dakika ya 84 baada ya wachezaji wa Argentina kupeana pasi hewa hisiyokuwa na macho na hatimaye Vedad Ibisevic kuwachoma bao akipewa pasi na Senad Lulic na kufanya 2-1.Vedad Ibisevic akiwachoma bao la kizembe Vedad Ibisevic akishangilia bao lake la dakika za mwishoni Zawadi yeu hii...1-0!!Aguero na mwenzake wakishangilia bao mapeeema huku wachezaji wa Bosnia-Herzegovina (kushoto) wakijiuliza!Lionel Messi akipongezwa baada ya kupiga frii kiki iliyosababisha mpaka Kolasinac kujifunga bao langoni mwao.Frii kiki iliyopigwa na Linel Messi katika dakika ya tatu na kutokea kujifunga bao kupitia kwa mchezaji wa Bosnia-Herzegovina Sead Kolasinac kujifunga bao na kuwapa zawadi ya bao la mapema dakika ya 3 Argentina.Mashabiki wa timu ya Argentina wakiipa sapoti timu yao usiku huu!! 
VIKOSI:
Argentina
: Romero, Zabaleta, Campagnaro, Federico Fernandez, Garay, Rojo, Maxi Rodriguez, Mascherano, Di Maria, Messi, Aguero.
Subs: Orion, Gago, Biglia, Perez, Higuain, Augusto Fernandez, Demichelis, Palacio, Alvarez, Lavezzi, Basanta, Andujar.

Bosnia-Herzegovina: Begovic, Mujdza, Bicakcic, Spahic, Kolasinac, Besic, Hajrovic, Pjanic, Misimovic, Lulic, Dzeko.
Subs: Fejzic, Vrsajevic, Vranjes, Ibisevic, Susic, Sunjic, Ibricic, Medunjanin, Visca, Hadzic, Salihovic, Avdukic.
Referee: Joel Aguilar (Slovakia)

Saturday, June 14, 2014


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa kuifadhili timu ya taifa ya soka Harambe Stars ziara ya kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la dunia Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo walikabidhiwa tiketi za ndege kwenda Brazil. Kitendo cha Rais bila shaka ni jambo la kutaka kuwatia motisha wachezaji wa timu ya taifa ambao hivi karibuni waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa moja katika duru ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika baadaye mwakani.Rais Kenyatta akiongea na Wachezaji wa Timu hiyo.
Hapa Akigawa tiketi huku akishuhudiwa na mkewe Bi. Margaret Kenyatta na seneta wa Nairobi Mike Sonko (kushoto).
Picha ya Pamoja.


Mchezaji wa Chile Gary Medel akimwendesha mchezaji wa Australia Tim Cahill
Mfungaji wa bao la kwanza wa Chile Alexis Sanchez  akimfunga kipa wa Australia Maty Ryan

Sanchez akishangilia bao lake la kwanza kwa Chile

Sanchez akishangilia bao lake la kwanza dhidi ya Australia..

Mauricio Isla akiteleza kumpongeza  Sanchez kwenye kona

Mchezaji wa  Chile Jorge Valdivia ndie aliyeifungia bao la pili na kufanya 2-0

Valdivia akipongezwa na Wachezaji wa Akiba
Wachezaji wote timu mbili  Chile na  Australia walianza kuimba nyimbo za Taifa za Nchi zao
VIKOSI:
Chile:
Bravo, Diaz, Mena, Jara, Isla, Vidal, Valdivia, Vargas, Medel, Alexis, Aranguiz.
Subs: Toselli, Albornoz, Silva, Carmona, Pinilla, Rojas, Orellana, Beausejour, Gutierrez, Fuenzalida, Paredes, Herrera.
Goals: Sanchez 12, Valdivia 14 J. Beausejour 90'+



Australia: Ryan, Milligan, Cahill, Franjic, Davidson, Leckie, Wilkinson, Spiranovic, Jedinak, Oar, Bresciano.
Subs: Langerak, Wright, Taggart, Halloran, Bozanic, Troisi, Holland, McKay, McGowan, Vidosic, Luongo, Galekovic.
Referee: Noumandiez Doue (Ivory Coast)

Darly Janmaat  na Diego Costa wakiendana sambambaWasley Sneijder akifanya yakeSergio akiwekewa kigingi na NigelDiego Costa vipi...unasababisha penati...Mzee Mzima Alonso ndie aliyeipa bao kwa mkwaju wa penati SpainXabi Alonso akishangilia baoVan Persie akitupia kusawazisha...1-11-1....Van Persie akimpagawisha kipa wa Spain kwa bao la kiwangoVan Persie akishangilia bao lake Nipe tano bosi wangu!! Nilikwambia!! leo ni chinja chinja!!Robben akitupia..Kipa Cassilas leo hii kama mtoto !!Mpaka ndani ya nyavu!! bao la tatuStefan akipeta baada ya kufunga baoVan Persie tena...Chupuchupu!!5-1

waliotembelea blog