Sunday, May 4, 2014


Vital: Dzeko (left) is congratulated by his team-mates after scoring the first of his goalsWakicheza Ugenini Goodison Park, Man City walitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuifunga Everton Bao 3-2 na kutwaa Uongozi wa Ligi Kuu England kwa kuwakamata Liverpool kwa Pointi na wao kuongoza kwa ubora wa Magoli huku Mechi zimebaki 2 Ligi kwisha. Game over: The Manchester City players join Dzeko in celebration of his second goalDakika ya 11 kipindi cha kwanza Everton walipata bao kupitia kwa Barkley baada ya kupiga mpira kwenye umbali wa yadi 25 na kuzama mpaka nyavuni mwa lango la Manchester City.
Dakika ya 22 Aguero alisawazisha bao  kwa timu yake City na kufanya 1-1. Lakini muda kidogo aliumia na kulazimika kutolewa nje na nafasi yake ilichukuliwa na Fernandinho katika dakika 28.Aguero akichekiwa na docta wa timu kuona kama ataendelea au la!!

Edin Dzeko dakika ya 43 anaongeza bao la pili na kufanya 2-1 dhidi ya wenyeji Everton na mpira kwenda mapumziko City ikiwa mbele ya bao 1.
Dakika mbili kupita kutoka mpira uanze kipindi cha pili dakika ya 47 City wakapata bao la tatu lililofungwa na Edin Dzeko tena na akifanya 3-1.Nice one! City goalkeeper Hart celebrates team-mate Edin Dzeko scoring their third goal of the gameKipa wa City nae alishangilia bao hilo!Edin Dzeko
Everton hawakubweteka walitafuta bao na dakika ya 65 Lukaku aliwapachikia bao na kubadilisha matokeo kuwa 3-2.

Ushindi huu wa bao 3-2 City wamepanda kileleni wakiwa na pointi 80 wakilingana na Majogoo Liverpool wakitofautiana mabao ya kufunga.Joy: The Everton players join Barkley as the team celebrate his brilliant first half strikerKipigo hiki kimeondoa matumaini ya Everton kucheza UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao na kuipa nafasi hiyo Arsenal.Bullet: Romelu Lukaku scored a brilliant diving header to give his side hope in the second halfLukaku akifunga bao la pili
Sasa City wamebakisha michezo miwili tuu nayo ni ya Nyumbani kwake Etihad msimu kumalizika, Timu hizo ni Aston Villa tarehe 7 mwezi huu wa tano na mechi ya mwisho ni tarehe 11 na watawakaribisha tena West Ham United.
michezo mingi kwa City itakuwa ya kujipima nayo itapigwa mwezi saba na wamepanga kucheza na Milan na Liverpool.


MABINGWA WATARAJIWA - MITANANGE WALIOBAKIWA NAYO!

CHELSEA
Mei 4: Chelsea v Norwich
Mei 11: Cardiff v Chelsea

LIVERPOOL 
Mei 5: Palace v Liverpool
Mei 11: Liverpool v Newcastle

MANCHESTER CITY 
Mei 7: City v Aston Villa
Mei 11: Man City v West  Ham United

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog