Mratibu
Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’,
Kareeem Omary ‘KO’ (kushoto) akiwa na familia ya marehemu Albert
Mangwea ‘Ngwair’ Mama mzazi wa Mangwea (Katikati) na kaka wa Mangwea,
Keneth Mangwea (kulia).
Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo la ‘Love Concert –Kumbukumbu ya Mangwea’, Kareeem Omary ‘KO’ .
Bana ya Love Concert
Taswira ya Nyumbani kwa Mama Mangwea kwa sasa.
Mangwea enzi za uhai wake
..Mastaa kibao kujumuika katika ‘LOVE CONCERT’
..Afande Selle, Belle 9, Samir na wengineo –Moro
P-Funky, Mswaki, Chemba Squad kutikisa
Na Andrew Chale
MASTAA mbalimbali nchini wakiwemo
wanamuziki wanatarajiwa kushiriki kwenye tukio maalum la kumbukumbu ya
mwaka mmoja tokea kifo cha marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ ,
litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nyumbani Park (Samaki samaki Spot) ,
Kihonda Morogoro mjini Juni 28.
Akizungumza na mtando huu ,
Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo, Kareeem Omary ‘KO’ alisema
maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila mwaka, limepwa jina
la ‘Love Concert – Kumbukumbu ya kifo cha Albert Mangwe’.
Kareem, aliwaomba wadau
kujitokeza kwa wingi kuunga mkono kwenye tukio hilo kwani litakuwa la
kipekee na la aina yake ambalo pia litatoa fursa kwa wakazi hao pia
mikoa jirani na watu kutoka nje ya Tannzania ambao watauzulia.
“Nawaomba wadau kujitokeza
kuonesha upendo wa pamoja. Kumbukumbu kwa mpendwa wetu kama ilivyo
utamaduni wetu.” alisema Kareem.
Na kuongeza kuwa, siku hiyo Watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa pamoja na mama mzazi wa Mangwea kama kumbukumbu.
Kareem aliwataja wasanii
watakaotoa burundani, ni pamoja na kutoka kwa kundi la Wanachemba
ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu Ngwair, JSqueezer, P Funky Majani
na Mswaki. Kwa upande wa wasanii kutoka Morogoro ni pamoja na Afande
Sele, Team Racers, Mc Koba Chris wa Marya, Belle 9, Samir, Zombie,
President Mirrow, Jordan wa Dejavu na wengine wengi.
Katika siku hiyo ya Juni 28,
ambayo ndiyo siku aliyopatwa na umati marehemu, Kareem alisema kabla ya
matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa na ibada mbili maalum ikiwemo ya
Kanisani na ile ya nyumbani.
Aidha, Kareem alisema katika
tukio hilo, ambalo linatarajia kuanza majira ya jioni ya saa 10 hadi saa
12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa burudani ikiwemo ya kuimba na
nyinginezo na baadae usiku wa kuanzia saa 2 hadi majogoo wasanii hao
mbalimbali watatawala jukwaa na burudani ya nguvu ya kumbukumbu.
Marehemu ‘Ngwair’ alifariki
dunia akiwa nchini Afrika kusini, alijizolea umaarufu kwa nyimbo kama
Mikasi na Nisikilize Mi na nyingine nyingi alizowahi shirikishwa na
wasanii mbalimbali nchini wakiwemo Professa Jay, Nuru, TID, Chidi Benz
na wengine wengi.