Na Mwandishi Wetu
Msanii wa
filamu za bongo Yusuph Mlela ameibukia katika mchezo wa masumbwi nchini
kwa kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya mchezo wa ngumi kama
vile Glove,Clip bandeji,Proctecta,GumShit kwa klabu ya msisili iliyopo
kinondoni Dar es salaam akizungumza mara baada ya kukabidhi msaada wa
vifaa hivyo Mlela alisema nimevutiwa na vijana wenzangu jinsi
wanavyojituma kufanya mazoezi hivyo nikaamua kujitolea kidogo nilicho
nacho kwa ajili ya kuendereza mchezo huu wa masumbwi katika
kata yangu ambapo mimi naishi karibu na maeneo haya hivyowalivyo niomba
nichangie nikawa sina jinsi kwa kuwa na mimi mwenyewe siku moja moja
nitakuwa nakuja kufanya mazoezi hapa hapa nawaomba wadau wengine wenye
uwezo zaidi yangu ata ambao wapo kama mimi wasaidie vijana kwa ajili ya
kujiendeleza na mchezo huu waupendao
Nae
kocha wa mchezo wa ngumi katika Klabu ya Msisiri Daudi Muhunzi alitoa
shuklani zake kwa Mlela kuwakumbuka vijana wenzie ambao walikuwa na
huaba wa vifaa vya ngumi kwani yeye amekuwa kama mkombozi katika kata
hiyo aliongeza kwa kusema tunaomba
wadau wengine waje watusaidie vifaa mbalimbali kama punch bag,pad na
maswala ya hudhamini wa muda mrefu kwa ajili ya kuendereza gym hii
ambayo tunaitumia kwa kuchangia kidogo
0 maoni:
Post a Comment