Thursday, March 20, 2014


KINYANG`ANYIRO cha ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014, bado kinabaki kuwa kitendawili kwa timu zilizopo juu katika msimamo.
Sare ya bao 1-1 jana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baina ya vinara Azam fc dhidi ya Yanga imezidi kuweka mazingira magumu kwa mabingwa watetezi, Young African.
Katika mchezo huo  uliovuta hisia za mashabiki, Yanga walikuwa wa kwanza kufunga bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Didier Kavumbagu, lakini Azam fc walisawazisha dakika za lala salama kupitia kwa kinda, Kevin Friday.
Hiyo ilikuwa mechi ya 19 kwa Yanga, wakati kwa Azam fc ilikuwa ya  20, huku wakijikusanyia pointi 44, wakati Wanajangwani wakivuna pointi 40 katika nafasi ya pili.
Yanga SC wamebakiza mechi 7, wakati Azam fc wamebakiza mitanange  6.
PICHA YA PG.24 
Mtatwaa Ubingwa? : Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la Didier Kavumbagu jana uwanja wa Taifa
Wikiendi hii timu zote zitashuka dimbani. Yanga watasafiri mpaka mkoani Tabora kuwafuata maafande wa Rhino Rangers, wakati jumapili machi 23, Azam fc watawakaribisha JKT Oljoro,  uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Rhino Rangers ndio wanaoburuza mkia katika msimamo wakiwa wameshacheza mechi 21 na kujikusanyia pointi 13 tu kibindoni.
Kwa asilimia kubwa, maafande hawa wa Tabora, wameshachungulia kushuka daraja na inawezekana hakuna muujiza wa kubaki ligi kuu msimu huu kwasababu ya mazingira yao.
_DSC0044 
Mchezo dhidi ya Yanga utakuwa mkali endapo bado Rhino wanahitaji ushindi.
Lakini imani yao imeshuka na wanacheza bora liende na wameshapoteza matumanini ya kuendelea kucheza ligi kuu.
Pointi 13 kwa mechi 21 ni chache sana, zinahitajika nguvu za ziada kushinda mechi zote 5 walizobakiza, hapo sasa tunaweza kuzungumza mengine.
Yanga wataingia uwanjani wakiwa ma matokeo ya sare ya jana na suluhu ya Mtibwa Sugar wiki iliyopita uwanja wa Jamhuri.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog