Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano
wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika
ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Machi 17, 2014. Picha na
OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimina na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Phillip Mangula, ambaye pia alikuwa ni miongoni mwa washiriki wa mkutano huo, mara baada ya kufungua mkutano huo kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia ukumbini humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalamu wa Kilimo, Maximillian Sarakikya, wakati alipotembelea banda la Kampuni ya Balton Tanzania, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Machi 17, 2014. Kulia ni Mkuu wa Maendeleo ya Biasara na Habari, Linda Byaba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipongezwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Janeth Mbene, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, Machi 17, 2014. Kulia ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi (wa pili kulia) ni Mwakilishi wa Ubalozi wa Israel kwa nchi za Tanzania, Kenya Uganda na Seychells, Gilad Millo.
Chanzo: The Habari
0 maoni:
Post a Comment