Picha
zifuatazo zinaonesha tukio la mshika kamera ya kuchukua matukio kwenye
ligi ya Ujerumani alivyopamiwa na mchezaji wa Hoffenheim, Andreas Beck
hadi kuzimia hapo hapo uwanjani. Baada ya tukio hili mshika kamera huyo
alipelewa haraka hospitali ili kufanyiwa matibabu zaidi. Kutokana na
tukio hili tayari mashirikisho ya mpira duniani yameanza kufanyia kazi
mfumo mzima wa kuweka kamera viwanjani ili kuepusha matukio kama haya
kutokea tena kwani ni hatari kwa usalama wa wachezaji na waandishi.
Mbali ya kupamiwa na wachezaji, waandishi pia wana hatari kubwa ya
kupigwa na mipira ya kasi kutoka uwanjani.
0 maoni:
Post a Comment