Sir
Alex Ferguson (katikati) akiwa amesimama na viongozi wa chuo cha Ulster
Ireland baada ya kupewa degree ya heshima kutokana na mchango mkubwa
aliyoutoa kwenye soka hususani Man utd. Katika maneno yake mbele ya
wanachuo 500 Sir Alex alisema ' Najivunia kupokea degree hii ya heshima
kutoka kwenye chuo kikubwa kama hiki. Ninayo furaha sana kuona hata chuo
kimeona mchango wangu na kufikiria kunipa tuzo. Hii ni ishara tosha
kuwa mafanikio yangu katika soka yatawahamasisha pia wanachuo ambao wana
ndoto ya kutimiza mambo makubwa kwenye maisha yao kwa kudumisha yale
niliyokuwa nayaamini kama chachu ya mafanikio ambayo ni bidii na tabia
njema'.
0 maoni:
Post a Comment