Wednesday, February 5, 2014

 


Wawakilishi wa Tanzania bara kwenye mashindano ya klabu Bingwa barani Afrika timu ya Young Africans itashuka dimbani siku ya jumamosi kuivaa timu ya Komorozine de Domoni ya Visiwa vya Comoro katika mchezo wa hatua ya awali ya Klabu Bingwa barani Afrika.
Young Africans itashukda dimbani kuhakikisha inaendeleza wimbi la ushindi kufuatia kupata ushindi katika mchezo wa mwisho dhidi ya timu ya Mbeya City mchezo ambao ulikuwa ni kuwasisimua kwa wapenzi wa soka nchini kwa ujumla.
Kikosi cha Young Africans chenye wachezaji 25 kimeweka kambi mjini Bagamoyo kujiandaa na mchezo huo ambapo wachezaji wake wote wapo katika hali nzuri na wakiendelea na maandalizi ya mchezo huo.
Kocha Mkuu wa Young Africans mholanzi Hans Van der Pluijm jana amekifanyisha kikosi chake mazoezi mara mbili asubuhi na jioni , huku leo akitarajia kuendelea na mazoezi jioni katika kuwaweka sawa kwa ajii ya mehci hiyo ya jumamosi.
Akiongelea mchezo wa jumamosi kocha Hans alisema anashukuru vijana wake wote wako fit, hakuna majeruhi hata mmoja na kikubwa wakiwa mjini Bagamoyo wanapata muda wa kupumzika mara baada ya mazoezi jambo ambalo kiafya ni muhimu.

Viingilio vya mchezo huo wa jumamosi ni:
VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/=
Orange Tshs 10,000/=
Blue & Green Tshs 5,000/=
Aidha tiketi zitaanza kuuzwa siku moja kabla ya mechi (ijumaa) katika vituo vifuatavyo:
Makao Makuu - Young Africans SC
Kariakoo - Sokoni
Shule ya Sekondari Benjamini - Uhuru
Mwenge - Stand
Oil Com - Ubungo
Steers - Mtaa wa Samora
Dar Live - Mbagala
Oil Com - Buguruni
Uwanja wa Uhuru - Chang'ombe
Kimara Mwisho - Stand

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog