H-Baba akikamua katika Tamasha kubwa la Ujasiriamali uko mwanza
Tamasha kubwa la Ujasiriamali lililofikia tamati jana jioni katika
Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza lilitawaliwa na elimu pamoja na
burudani kali kutoka kwa wasanii Fid Q, H-Baba, Young Killer na Jitta
Man. Kwa upande wa injili, burudani hizo ziliongozwa na Martha Mwaipaja
na Emmanuel Mgaya 'Masanja Mkandamizaji. Walimu wa ujasiriamali nchini,
Eric Shigongo na James Mwang'amba wakiwa sambamba na Mbunge wa Mbeya
Mjini (Chadema), Mhe. Joseph Mbilinyi 'Sugu' walitoa elimu ya
ujasiriamali kwa wakazi wa Mwanza na kuwaacha wakiwa wameiva kwenye
masuala hayo.
0 maoni:
Post a Comment