MSHAMBULIAJI
nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amefungua jumba lake la
makumbusho katika mji aliozaliwa ambapo amesema ameacha nafasi kwa tuzo
ya Ballon d’Or na mataji mengine mengi atakayopata. Akiwa amesimama
pembeni mwa tuzo yake ya Ballon d’Or aliyopata mwaka 2008 na tuzo
zingine 125 alizopata peke yake au na timu tangu alipoanza kucheza soka,
Ronaldo mwenye umri wa miaka 28 aliwaambia waandishi wa habari kuwa
jumba hilo la makumbusho aliloliita CR7 ni zawadi kwa mashabiki wake.
Ronaldo
amesema anajivunia siku hiyo muhimu na pia ameacha nafasi kwa ajili ya
tuzo zingine atazoshinda kabla hajaamua kutundika daluga rasmi.
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA limemtaja Ronaldo, Lionell Messi na
Franck Ribery kugombea tuzo ya Ballon d’Or mwaka huu ambayo zamani
ilikuwa ikijulikana kama tuzo ya mchezaji bora wa dunia wa mwaka.
Ronaldo na mpenzi wake Irina Shayk wakiingia kwenye jumba hilo linaloitwa CR7
Ronaldo stands by a golden boot in the museum
Ronaldo addressed the media after the unveiling of his brand new waxwork
0 maoni:
Post a Comment