Sunday, September 22, 2013


 
  
Baadhi ya majeruhi katika shambulio la kigaidi jijini Nairobi.
-Wadai Kenya ilipuuza onyo lao
-Wasema ni kulipiza kisasi kwa Kenya kijihusisha katika vita ya Somalia

-Watu zaidi ya 30 wadaiwa kupoteza maisha wengine wakijeruhiwa

KUNDI la Alshabaab, limethibitisha kuhusika na shambulio la kigaidi lililotokea jana kwenye jengo la ghorofa nne lenye maduka la Westgate jijini Nairobi, nchini Kenya.
Alshabaab kupitia kwa afisa wake mmoja, imethibisha hilo na kueleza kuwa shabulio lilikuwa na kulipiza kisasi baada ya Kenya kujihusisha na vita ya Somalia.

 
Hali ilivyokuwa ndani ya jengo lililovamiwa na magaidi.
Walioshuhudia tukio hilo wanadai watu waliovalia magwanda yalioonekana kama ya kijeshi huku wengine wakiwa wamefunika nyuso zao walivamia jengo hilo huku wakifyatua risasi.
Maduka hayo ya Westgate hutendelewa sana na matajiri pamoja na wageni kutoka nchi mbalimbali.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, Al Shabaab imesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na kuendelea kuwaua waislamu wasio na hatia nchini Somalia, na shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
Taarifa kutoka Ikulu ya nchini Kenya, zinadai kuwa mmoja wa watuhumiwa aliyekamatwa katika tukio hilo  alifariki kutokana na majeraha yake.
Magaidi wapatao kumi walivamia jengo la kifahari la Westgate jana mchana la kuwapiga risasi kiholela Wakenya waliokuwa wanaendelea na shughuli zao za kawaida.




              WATU waliokuwa na silaha wamefyatua risasi mjini 
Nairobi, Kenya, kwenye eneo la maduka katika mtaa wa Westlands.
Walioshuhudia tukio hilo, wanasema kuwa maguruneti piya yalitumika.
Inaarifiwa watu watano wamekufa.(P.T)

Mwandishi wetu mjini Nairobi anaeleza kuwa washambuliaji
 inaarifiwa walivaa vilemba kama vya al-Shabaab, lakini
 haikuthibitishwa kama wapiganaji hao wamehusika.
Polisi waliojihami kwa silaha wamezingira jengo la maduka
 liitwalo Westgate, katika mtaa wa Westlands, na kuna taarifa
 ya watu waliojeruhiwa wakitolewa hapo kwa machera.














1 comment:

  1. UO NDO UISLAM ALIO URETA MUHAMAD KUTOKA KWA MUNGU WAKE WA AINAYAKE

    ReplyDelete

waliotembelea blog