Tuesday, August 13, 2013




Chuo kilichopo mji wa Nsuka kimeshuhudia tena mauaji ya kikatili ya dereva wa tipa ambae amewapa mimba mjane na mtoto wake. Ripoti inasema dereva huyo amechomwa moto na mtoto wa kiume wa mjane huyo,Sunday Ugwoke.

 Kutokana na habari zilizokusanywa  Sylvester Ezema alikuwa amejishikiza kwenye kampuni ya Ferguso Nig. Limited huko Akpa Edem na alikokuwa anaishi  alikuwa anashea fensi ya kawaida tu na mpenzi wake mjane. Taarifa zinasema kuwa alikuwa pia na mahusiano ya kimapenzi na mtoto wa kike wa mjane huyo ambaye alikuwa hajui mpaka alipofariki siku chache zilizopita ndipo alipokuja kujua.

Sylvester alichomwa moto mpaka akafa na Sunday ambaye alishamwonya aachane na mama yake na aache kufanya nae mapenzi kwenye chumba cha marehemu baba yake,ambacho kimepakana na chumba chake,Onyo ambalo marehemu Sylvester hakulizingatia na kuendelea na tendo hilo baya.
Sylvester aliyapa kisogo maonyo ya Sunday akisema kuwa huyo mjane ni 'family friend' so hakuna atakayewashitukia. Kwa kutofuata maonyo,siku moja Sunday,alijikoki na pilipili ya kusagwa na petrol akamvamia yule 'lover boy'. Sylvester alipotoka tu mlangoni kwake, Sunday alimmwagia pilipili na petrol kisha akamuwasha  moto.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog