Leo tunawaletea mkusanyiko wa mambo kumi toka kwa mwigizaji mkongwe nchini Vicent Kigosi (Ray) kuhusu maisha na namna ambayo anafikiri kuhusu maisha ya kila siku ya mwanadamu.
Maoni haya tumeweza kuyapata baada ya kufanya uchambuzi yakinifu kwenye akaunti mbalilmbali za mwigizaji huyu za kwenye miandao ya kijamii na kuzipanga kwa jinsi ambavyo tunaona stahili. Soma hapo chini ujue mwigizaji huyu huwa anawaza nini kuhusu maisha.
- Mungu ndio kila kitu katika dunia hii
- Amani ndio kitu cha msingi kwenye nchi yetu ya Tanzania
- Mungu ni mwema sana katika maisha ya binadamu
- Ukiwa na uwezo wa pesa ishi na watu vizuri
- Pambana kijana na maisha wakati wako ndio huu
- Hakuna kitu muhimu duniani kama kuwekeza kwa jamii
- Mazoezi ni bora kwa afya yako
- Pole pole ndio mwendo ukiwa na haraka waweza kujikwaa
- Kama unapata kumi kwanini usipate na mia?
- Mwisho wa ubaya ni aibu
0 maoni:
Post a Comment