Leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya na biashara
haramu ya dawa hizo. Umoja wa Mataifa umeitenga siku hii kuuhimiza
ulimwengu kupambana na janga hili ambalo linaathiri hasa vijana kote
duniani.
Ni jukumu la kila mmoja kupambana na dawa
Bado kiwango cha matumizi ya dawa kama vile Heroin, cocaine na
amphetamine hakijashuka lakini mtindo huu wa kuwepo kwa aina mpya za
dawa za kulevya unatia wasiwasi.
Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya watu walioambukizwa virusi vya HIV
kupitia kujidunga sindano miongoni mwa waraibu wa dawa za kulevya
ilikuwa milioni 1.6 mwaka 2011.
0 maoni:
Post a Comment