Friday, July 5, 2013

Papa Francis
Wachambuzi wanasema kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis ameongeza nguvu zaidi katika kushughulikia kashfa zilizoigubika benki ya Vatican kwa kumuondoa viongozi wa juu wa tasisi hiyo.
Paolo Cipriani na Massimo Tulli, mkurugenzi na naibu wake katika benki hiyo ya Vatikan walitoa rasmi barua za kujiuzulu kwao jumatatu iliyopita kwa maslahi ya taasisi hiyo na makao makuu ya kanisa hilo kwa ujumla. Rais wa benki ya Vatican Ernst von Freyberg, amepokea maamuzi hayo kwa ili kufanikisha upatikanaji wa viongozi wapya kwa lengo kuifanya benki hiyo kukidhi vigezo vya kimataifa dhidi ya uwekezaji wa fedha haramu.
Wataalamu wa masuala ya kidini na mahakama wamesema makao makuu ya kanisa Katoliki Vatican yamelazimika kuwaondoa maafisa wawili ambao walinusurika katika sakata lililomuondoa mkuu wa zamani wa benki hiyo, Ettore Gott Tedeschi, alishutumiwa kwa uongozi duni lakini pia kugubikwa na ripoti ya uwekezaji wa fedha haramu.


Hatua muhimu ya Vatican
waumini wakihudhuria misa iliyoongozwa na Papa Francis
  

Kwa mujibu wa mtaalamu, Fionrena Sarzanini kufukuzwa kwao ni hatua muhimu kwa Vatican kwa kuwa viongozi hao waliojiuzulu Cipriani na Tuli wapo katika orodha ya watu wanaofuatiliwa na tume ya waendesha mashitaka ya Roma iliyoundwa mwaka 2010 kwa ajili ya kuchunguza madai ya fedha haramu.
Fiorenza amesema uchunguzi huo uliopangwa kumalizika katika kipindi cha siku chache zijazo ungalipenda kuona wakishitakiwa kutokana na shutuma za kuruhusu vitendo haramu kufanyika. Mbali na hayo mkurugenzi huyo na naibu wake waliojizulu hivi karibuni wanahusishwa pia kuwa na uhusiano wa karibu na Nunzio Scarano, ambae amefanya kazi kama muhasibu mwandamizi wa benki ya Vatican ambae alikamatwa ijumaa iliyopita kwa tuhuma za njama za kusafirisha fedha haramu kutoka Uswis na kuziingiza nchini Italia.
Mtaalamu mwingine wa masuala ya kidini Marco Politi amesema pamoja na kuwepo kwa minong'ono kwamba makaoa makuu ya kanisa katoliki yanataka kuachana na taasisi hiyo kabisa lakini Papa Francis anaonekana si mwenye nia ya kufanya hivyo kutokana na umuhimu wa ke kwa utendaji wa majukumu ya kanisa.
Kutokana na mfululizo wa taarifa za vyombo vya habari vya Italia kuhusu kuwepo kwa akaunti ambazo wamiliki wake hawajulikani zinazotumiwa na wafanya uhalifu wa kupanga na wanaosafarisha fedha kwa njia za haramu taarifa nyingi zaidi zinatarajiwa kuwekwa hadharani kuhusu utendaji wa benki hiyo.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog