Thursday, April 27, 2017


Maruane Fellaini ameondeshwa kadi nyekundu baada ya kumpiga kichwa mchezaji wa City Kun Aguero huku akiwa na kadi ya njano kipindi cha pili. Pia mchezo huo uliomalizika bila ya kufungana kwa kutoka 0-0 umekuwa ni afueni kwa Man United kwa kuendeleza mechi nyingi bila kufungwa msimu huu. Na huku wakionekana kupanda kujihakikishia kuwa kwenye nafasi ya kugombea nafasi ya nne bora ili kucheza Klabu Bingwa msimu ujao. Man City v Man Utd, EPL MANCHESTER DERBY LIVE scoreVIKOSI: 
MAN CITY: Bravo, Zabaleta, Kompany (C), Otamendi, Kolarov, Fernandinho, Yaya Toure, Sterling, De Bruyne, Sane, Aguero
Akiba:
Caballero, Sagna, Fernando, Navas, Clichy, Gabriel Jesus, A. Garcia

MAN UNITED: De Gea, Valencia, Blind, Bailly, Darmian, Carrick, Herrera, Fellaini, Mkhitaryan, Martial, Rashford.
Akiba: Romero, Shaw, Fosu-Mensah, Tuanzebe, Young, Lingard, Rooney



Sunday, April 23, 2017

Baada ya kuondolewa katika michuano ya UEFA Champions League kwa timu ya FC Barcelona usiku wa April 23 2017 walisafiri hadi katika jiji la Madrid kuendeleza harakati zao za kuwania Kombe la LaLiga kwa kucheza dhidi ya wapinzania wao wa jadi Real Madrid katika uwanja wa Santiago Bernabeu.
Mastaa wa zamani wa Real Madrid Ronaldo de Lima na Luis Figo walikuwepo uwanjani kuangalia game.
FC Barcelona walisafiri kuelekea Madrid tayari wakiwa wanamkosa mchezaji wao wa kimataifa wa Brazil Neymar kutokana na kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, licha ya kumkosa Neymar safu ya ushambuliaji ya Barcelona bado ilikuwa imara na kupelekea kupata ushindi wa magoli 3-2.
Lionel Messi akifunga goli lake la 500 akiitumikia FC Barcelona
Lionel Messi ndio ameonekana kuwa hatari zaidi kwa kumsababishia Sergio Ramos kupata kadi nyekundu ya 22 katika historia yake ya soka kutoka na kumchezea Lionel Messi faulo dakika ya 77, Lionel Messi ndio alikuwa hatari na kufanikiwa kufunga magoli mawili dakika ya 33 na 90 baada ya Ivan Rakitic kufunga goli la pili dakika ya 73.

Wakati magoli ya Real Madrid yalifungwa na Casemiro dakika ya 28 na James Rodriguez dakika ya 85 akitokea benchi, ushindi huo wa FC Barcelona unavunja rekodi yaa Real Madrid ambao walikuwa wamecheza mechi 22 bila kufungwa katika uwanja Santiago Bernabeu toka February 27 2016.
Barcelona anaongoza baada ya ushindi wa leo kwa tofauti ya magoli lakini amemzidi mchezo mmoja Real Madrid

Thursday, April 6, 2017



Premier League
PosLogo &TeamPWDLGDPts
1ChelseaChelsea3023343872
2Tottenham HotspurTottenham Hotspur3019833865
3LiverpoolLiverpool3117952760
4Manchester CityManchester City3017762358
5ArsenalArsenal2916672554
6Manchester UnitedManchester United29141231954
7EvertonEverton3114981951
8West Bromwich AlbionWest Bromwich Albion3112811-144
9SouthamptonSouthampton2910712-137
10WatfordWatford3010713-1237
11Leicester CityLeicester City3010614-1036
12Stoke CityStoke City319913-1236
13BournemouthBournemouth319814-1235
14BurnleyBurnley3110516-1235
15West Ham UnitedWest Ham United319616-1633
16Crystal PalaceCrystal Palace309417-1131
17Hull CityHull City318617-2930
18Swansea CitySwansea City318419-2928
19MiddlesbroughMiddlesbrough3041115-1523
20SunderlandSunderland305520-2920

Wednesday, April 5, 2017



Mchezaji anayetaka kuondoka Yanga Ruksa, Mlango wazi
Uongozi wa Yanga umeweka bayana kwamba hauna mpango wa kumzuia mchezaji yeyote kuondoka iwapo atahitaji kuihama klabu hiyo
Mabingwa watetezi Ligi Kuu Bara, Yanga SC ambao ndio wanaoongoza kwenye msimamo wa ligi msimu huu kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya mahasimu wao Simba huku kila timu ikibakiwa na mechi tano kumalizika, wamtamka kuwa mchezaji yeyote anayetaka kuondoka mwisho wa msimu mlango uko wazi.
Kuelekea mwisho wa msimu Uongozi wa Yanga umetoa ruhusa kwa mchezaji yoyote kuondoka Yanga iwapo tu atafuata taratibu, Katibu wa Yanga Boniface Mkwasa alisema.
“Kama kuna Mchezaji anataka kuondoka basi awe muungwana, atueleze mapema na taratibu zifuatwe, Pia kama kutakuwa na mchezaji ambaye Mwalimu anona hamuhitaji sisi tutafuata taratibu na kumueleza mapema kabisa.” Alisema katibu huyo wa Yanga kwa mujibu wa Shaffih Dauda Blog.
Wakati akiyasema hayo Mkwasa kuna hatari timu ya Yanga ikawakosa wachezaji wengi muhimu ambao mikataba yao inaelekea kuisha ndani ya Yanga, Wazimbambwe wawili Donald Ngoma na Thabani Kamusoko wanaelekea kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu na uongozi wa klabu hiyo haujaweka bayana kuhusu kuwaongezea mikataba mipya.
Pia mabeki wa kati wazawa Kelvin Yondani na nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ mikataba yao inafikia tamati mwisho wa msimu, kadhalika kwa mshambuliaji Anthony Mateo na beki wa kimataifa wa Togo Vicent Bossou.
Kwa sasa wapo katika maandalizi kwa ajili ya mechi ya kombe la shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger katika uwanja wa Taifa na watarudiana wiki moja baadaye huko Algeria.

Tuesday, April 4, 2017


EPL RATIBA
Jumanne Aprili 4

2145 Burnley v Stoke City
2145 Leicester City v Sunderland
2145 Watford v West Bromwich Albion
2200 Manchester United v Everton


MANCHESTER UNITED Jumanne Usiku wako kwao Old Trafford kucheza na Everton kwenye Mechi ya EPL, Ligi Kuu England, ambayo hiyo na ile inayufuatia Wikiendi inayokuja dhidi ya Sunderland ndiyo itatoa mwelekeo wa Timu hiyo kuwemo 4 Bora au la kwa mujibu wa Meneja wao Jose Mourinho.

Akiongelea kuelekea Mechi hii na Everton, Mourinho alisema atashusha Kikosi kikali dhidi ya Everton na Sunderland na matokeo ya Mechi hizo ndio yataamua nini hatima yao kwenye Ligi na kwani baada ya hapo watacheza Robo Fainali ya UEFA EUROPA LIGI na mkazo utakuwa huko.
Kufuzu 4 Bora ya Ligi kutawawezesha Man United kucheza UCL, UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu ujao lakini pia kutwaa EUROPA LIGI kutawapa nafasi hiyo pia.

Hivi sasa kwenye EPL Man United wapo Nafasi ya 5 wakiwa na Pointi 53 kwa Mechi 28 wakati Man City wapo Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 58 kwa Mechi 29.
Uso kwa Uso
-Man United hawajafungwa katika Mechi 4 zilizopita na Everton.
-Katika Mechi 49 za EPL, Man United Ushindi 33 Sare 8 Everton Ushindi 8
Man United wataingia Mechi hii wakitoka Sare ya 0-0 na West Bromwich wakati Everton walichapwa 3-1 na Liverpool Mechi zote zikichezwa Juzi Jumamosi.
Sare hiyo kwa Man United imeendeleza wimbi lao la Mechi 19 kutofungwa kwenye Ligi.

Hali za Vikosi:
Man United inategemewa kuwa nao tena Mfungaji wao Bora Zlatan Ibrahimovic na Kiungo Ander Herrera baada ya kumaliza Vifungo vyao vya Mechi 3 na 2 lakini itawakosa Majeruhi Juan Mata, Chris Smalling na Phil Jones huku pia kukiwepo uwezekano wa Paul Pogba kucheza baada ya kupona maumivu yake na kuanza mazoezi.
Everton inakabiliwa na Majeruhi 6 wakiwemo Seamus Coleman, alievunjwa Mguu akiichezea Nchi yake Republic of Ireland dhidi ya Wales Wiki ilyopita na pia Sentahafu wao wa Argentina Ramiro Funes Mori alieumia vibaya Goti.

Pia Mchezaji wa zamani wa Man United Kiungo Morgan Schneiderlin na Winga Aaron Lennon watakosekana kwa kuwa na maumivu.

Mechi ya Kwanza Msimu huu
Mapema Mwezi Desemba Zlatan Ibrahimovic aliifungia Bao Man United na Everton kusawazisha Dakika za lala salama kwa Penalti tata iliyotolewa kwa Rafu iliyofanywa na Mchezaji wa zamani wa Everton Marouane Fellaini na Adhabu hiyo kufungwa na Leighton Baines na kuifanya Gemu iishe 1-1.



Wanasayansi wa Chuo Kikuu cha Ghent nchini Ubelgiji wamegundua njia mpya ya kutengeneza mafuta ya kuendeshea gari kwa kutumia majani ‘Biofuel’ ambapo kwa mujibu wa wanasayansi hao, majani yana uwezo wa kutengeneza kiwango kikubwa cha ‘decane’ ambacho hutumika katika kuzalisha mafuta.
Akizungumza na Science Daily, Professa Way Cern Khor alisema: >>> “Majani yamekuwa yakitumika kulisha wanyama lakini pia yanaweza kuzalisha mafuta ‘Biofuel’ kwa kiasi kikubwa. Hii inaweza kuja kusaidia kupunguza bei ya mafuta. Tunafurahi kuweza kubadilisha kitu kisichotumika na kuwa nishati muhimu.”
Prof. alielezea jinsi atakavyoweza kuyabadilisha majani na kuwa mafuta ya gari akisema kuwa majani hayo yatawekwa bakteria maalum watakaoweza kuondoa sukari iliyopo ndani yake na kubadilika kuwa katika asidi ya lactic na caproic ambayo inatumika kutengeneza mafuta.
Hadi sasa wanasayansi hao wameweza kutengeneza kiasi kidogo cha mafuta kinachotokana na majani lakini jitihada zinaendelea kuweza kubadilisha majani kuwa katika hali ya kimiminika.

Monday, April 3, 2017



Moja kati ya majina yaliojipatia umaarufu na heshima kubwa katika soka ni Zinedine Zidane na Ronaldinho ambao uwezo wao umeifanya dunia ya soka kutokusahau mchango wao, Zidane ni mahiri katika kucheza mpira na kufanyia mbwembwe kama ilivyo kwa Ronaldinho.
Naomba nikusogezee video yao kila mmoja akionesha uwezo wake katika soka, mtu wangu wa nguvu naomba jikumbushe halafu usisahau kuacha comment yako nani unamkubali zaidi katika umahiri wa kuuchezea mpira.

waliotembelea blog