Tuesday, December 6, 2016




Baada ya kufariki uwanjani kwa mshambuliaji wa timu ya Mbao FC Ismail Khalfan siku ya Jumapili ya December 4, leo December 6 2016 imetoka ripoti ya kilichosababisha kifo cha mchezaji huyo wakati wa mchezo kati ya Mbao FC dhidi ya Mwadui FC.

Ripoti iliyotolewa na hospitali ya mkoa wa Kagera kuhusiana na kifo cha mchezaji huyo, kupitia kwa jeshi la Polisi, Ismail alifariki uwanjani kutokana na kumpata tatizo la kusimama ghafla kwa moyo (sudden Cardiac Arrest-SCA).

Kamishina Msaidizi wa Kagera, Augustin Ollomi ametoa taarifa baada ya uchunguzi wa madaktari kuhusu kifo cha mchezaji huyo ambaye hakuwa na jeraha lolote walibaini kusimama ghafla kwa moyo (sudden cardiac arrest) kulisababisha kifo

SUDDEN CARDIAC ARREST-SCA
Kwa faida yako msomaji:
Kawaida moyo una mfumo wa umeme (heart electrical system), ambao unadhibiti mapigo ya moyo, mfumo huu ukisimama basi moyo unashindwa kusukuma damu sehemu muhimu kama ubongo na ogani kuu.

Moyo ukisimama bila kurudi katika hali yake unasababisha kifo ndani ya sekunde chache na njia pekee ya msaada ni kupita electrical shock ili kushtua mfumo wa umeme wa moyo, na hii inapaswa kufanyika ndani ya sekunde chache mno.
CHANZO: salehjembe

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog