Tuesday, August 11, 2015



sterling 5
Winga wa Manchester City, Raheem Sterling ambaye amejiunga na timu hiyo baada ya kununuliwa toka Liverpool ameonekana kuanza kuwavutia mashabiki wa klabu yake mpya baada ya kitendo chake cha kugawa jezi kwa shabiki mdogo baada ya mchezo wake wa kwanza kwenye ligi kuu ya England.
Sterling ambaye alinunuliwa katika dili la paundi milioni 49 alivua jezi yake baada ya mchezo dhidi ya Westbromwich Albion na kwenda moja kwa moja jukwaani ambapo aliikabidhi jezi hiyo kwa shabiki mmoja ambaye alionekana kufurahia kitendo hicho.
Sterling akiruka uzio kwenda kutoa jezi kwa shabiki wa Man City.
Sterling akiruka uzio kwenda kutoa jezi kwa shabiki wa Man City.
Sterling alifanya kitendo hicho kwenye mchezo ambao Man City ilishinda kwa matokeo ya 3-0 matokeo ambayo yamewafanya waongoze ligi katika wiki yake ya kwanza huku mabingwa watetezi wa ligi hiyo Chelsea wakibanwa mbavu.
Sterling alivua jezi yake na kwenda kuigawa kwa shabiki wa Man City.
Sterling na jezi yake mkononi akiipeleka kwa shabiki wa Man City.
Shabiki aliyepewa jezi na Raheem Sterling akionyesha furaha yake.
Shabiki aliyepewa jezi na Raheem Sterling akiionesha huku akifurahia.
sterling 6

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog