Wenyeji Chile wametwaa Taji lao la kwanza kabisa baada ya kuibwaga Argentina kwa Penati 4-1 kufuatia Sare ya 0-0 katika Dakika 120 za Fainali ya Copa America, Kombe la Mataifa ya Marekani ya Kusini, iliyochezwa mbele ya Halaiki ya Mashabiki ndani ya Estadio Nacional Santiago Jijini Santiago.
Kipigo hiki kimeendeleza ukame wa Argentina wa Miaka 22 wa kutotwaa Taji lolote tangu walipobeba Copa America Mwaka 1993 huko Ecuador na pia unamfanya Kepteni wao Lionel Messi, aliewahi kuwa Mchezaji Bora Duniani mara 4, aendelee kutokuwa na mafanikio yeyote na Le Albiceleste tofauti na akiwa na Klabu yake FC Barcelona ya Spain.
Kwa Chile, ushindi huu umemaliza Karne yao ya kushiriki Mashindano bila Taji lolote baada ya kufanikiwa kufika Fainali 4 za Copa America, zile za 1955, 1956, 1979 na 1987, na kufungwa zote.
Chile, chini ya Kocha toka Argentina Jorge Sampaoli, hawakucheza Soka la kuvutia na walikosa nafasi moja ya wazi katika Dakika za Nyongeza 30 wakati Argentina, chini ya Kocha Gerardo 'Tata' Martino, nao walikosa nafasi ya wazi wakati Gonzalo Higuain alipokosa ndani ya Dakika 90.Ushindi! 4-1 kwa mikwaju ya penatiBalaa!! Alexis Sanchez alipowafungia mkwaju wa UshindiAlexis Sanchez akishangilia baada ya kuitoa ArgentinaMikwaju ya penati ikiendelea..Kipa wa Chile Claudio bravo akiwa amebeba juu zawadi yake ya Golden Grove Eduardo Vargas akiwa na mwanae pamoja na Tuzo yake
Ni shida!! Lionel Messi akiwa hoi kwa mara nyingi akichemsha ndani ya Fainali! Ukame waendelea...Choka mbaya!Shangwe kwa kwenda mbele huku ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwa wenyeji Chile
Baadhi ya Wachezaji wa Chile wakipeta baada ya kushinda kwa mikwaju ya penati dhidi ya Argentina.Argentina wameshindwa kutamba mbele ya Chile kwenye mchezo wa Fainali wa Copa America na kufungwa kwa mikwaju ya penati 4-1 baada ya kutoshana nguvu dakika 120 kwa kutoka 0-0.TASWIRADakika 120 zilimalizika bila kufungana tena kwa kutoka 0-0 na mikwaju ya penati kupigwa!Dakika 90 zilimalizika bila kufungana na kuongezwa muda wa dakika 30!Angel Di Maria akubali yaishe mapema kipindi cha kwanza! Lavezzi alichukuwa nafasi yakeKipindi cha pili kinaendelea..Mashabiki wenyeji chile!VIKOSI:
Argentina Wanaoanza: Romero, Zabaleta, Demichelis, Otamendi, Rojo, Biglia, Mascherano, Pastore, Messi, Aguero, Di Maria
Chile wanaoanza: Bravo, Isla, Medel, Silva, Beausejour, Aranguiz, Diaz, Vidal, Valdivia, Sanchez, Vargas
Chile vs Argentina, Estadio Nacional, Santiago
MashabikiNi Patashika Fainali Usiku huu Copa America kati ya Chile v ArgentinaChileLionel Messi kufanya kazi ya ziada punde!
0 maoni:
Post a Comment