Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akizungumza na wanamichezo
(hawapo pichani) kabla ya kuanza fainali ya Kombe la Chikawe katika
Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya
Marambo na Timu ya Motisha kutoka Kata ya Kilimanihewa zilipambana na
Timu ya Black Fire iliibuka mshindi kwa magoli 3 kwa 1. Kulia ni Mkuu wa
Wilaya ya Nachingwea, Pololeti Mgema.
Kapteni wa Timu ya Black Fire,
Ally Njaidi (kulia) akipokea fedha taslimu Shilingi 500,000 pamoja na
Kikombe cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti
Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo hilo,
ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe. Timu
hiyo iliirarua timu ya Motisha mabao 3 kwa 1 katika mchezo uliofanyika
katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu Mwalimu, naye
alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa na Mbunge
Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea akimsalimia mchezaji wa
Timu ya Black Fire, Faraji Mohamed wakati alipokuwa anaikagua timu hiyo
kabla ya fainali ya Kombe la Chikawe ambayo yalifanyika katika Uwanja wa
Sokoine, mjini Nachingwea. Timu ya Black Fire kutoka Kata ya Marambo
iliibuka kidedea baada ya kuinyuka Timu ya Motisha, Kata ya Kilimani
magoli 3 kwa 1. Nyuma ya Waziri Chikawe ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,
Pololeti Mgema.
Kapteni wa Timu ya Motisha,
Saidi Chakupewa (kulia) akipokea zawadi ya ushindi wa pili, kikombe na
fedha taslimu Shilingi 200,000 kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,
Pololeti Mgema, baada ya kumalizika fainali ya Kombe la Mbunge wa Jimbo
hilo, ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Timu hiyo ilifungwa na Timu ya Black Fire mabao 3 kwa 1 katika mchezo
uliofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Kushoto ni Naibu
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salimu
Mwalimu, naye alihudhuria fainali ya mashindano hayo ambayo yalianzishwa
na Mbunge Chikawe jimboni humo kwa kushirikisha timu 178 katika jimbo
hilo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (aliyevaa
kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Black Fire ambao ndio waliibuka
washindi. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Pololeti
Mgema.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (aliyevaa
kofia) akiwa na wachezaji wa timu ya Motisha kutoka Kata ya
Kilimanihewa. Kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea,
Pololeti Mgema.
Msanii maarufu wa bongofleva,
Seleman Jabir ‘Msaga Sumu’ akitumbuiza katika fainali ya Kombe la
Chikawe lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine mjini Nachingwea. Katika
fainali hiyo, Timu ya Black Fire iliibuka kidedea baada ya kuifunga timu
ya Motisha magoli 3 kwa 1.
Mchezaji wa timu ya Black Fire
(kulia) akisakata kabumbu katika fainali ya kombe la Mbunge Chikawe
lililofanyika katika Uwanja wa Sokoine, mjini Nachingwea. Timu hiyo ya
Black Fire iliinyuka timu ya Motisha magoli 3 kwa 1. Picha zote na Felix Mwagara.