Allardyce, maarufu kama Big Sam, alijiunga na West Ham 2011 wakati Timu hiyo iko Daraja la chini la Championship na kuirudisha Ligi Kuu England na Msimu huu walianza vizuri tu lakini mwishoni walififia na kumaliza Nafasi ya 12.
Wenyeviti wenza wa West Ham, David Sullivan na David Gold, wametoa shukran zao kwa Allardyce na pia kutamka kuwa wanayo Listi ya Watu wanaofaa kushika wadhifa huo wa Meneja.
Akiongea mara baada ya Mechi hiyo, Big Sam alisema uamuzi huu ni bora kwa kila upande.
West Ham ilikubali kichapo kwenye mtanange wa kumalizia Msimu wa Ligi Kuu England 2014-2015 ambapo West Ham ilichapwa 2-0 huko Saint James Park na Newcastle ambao ushindi huo umewabakisha Ligi Kuu England, Klabu ya West Ham imetangaza kusaka Meneja mpya baada kuamua kutoongeza Mkataba wa Meneja wao Sam Allardyce. Ametamka: "Nadhani ni sahihi kwa kila upande, kwangu na Klabu. Nilitimiza kila kitu walichonitaka, na nilifurahia hilo!"
0 maoni:
Post a Comment