Tuesday, May 26, 2015


Norwich City Leo hii wamefanikiwa kurudi tena Ligi Kuu England baada ya kuporomoka Msimu mmoja uliopita baada ya kuichapa 2-0 Middlesbrough
kwenye Fainali ya Mchujo wa Timu 4 za Daraja la Championship iliyochezwa Uwanjani Wembley Jijini London.
Mbele ya Watazamaji 85,656, Norwich City walipiga Bao zao 2 ndani ya Robo Saa ya Kwanza kwa Bao za Cameron Jerome alietumia vyema makosa ya Daniel Ayala na kufunga na kisha katika Dakika ya 15 Nathan Redmond alipiga Bao la Pili.

Norwich City, ambao walimaliza Ligi ya Championship Nafasi ya 3 na hivyo kukosa nafasi ya kupanda Ligi Kuu England moja kwa moja, kwenye Nusu Fainali ya Mechi hizi za Mchujo waliibwaga Ipswich Town Jumla ya Mabao 4-2 katika Mechi mbili.Boro walitinga Fainali hii kwa kuichapa Brentford Jumla ya Mabao 5-1 katika Mechi mbili.
Norwich City sasa wameungana na Bournemouth na Watford, ambazo zilimaliza Nafasi mbili za juu za Ligi ya Championship na kupanda Daraja moja kwa moja, kucheza Ligi Kuu England Msimu ujao kuzibadili Hull City, QPR na Burnley zilizoporomoka Daraja.
Mashabiki wa BoroTimu zikiingia Uwanjani WembleyKikosi cha NorwichKipute kimeanza ...mchezaji wa Boro chiniJerome ndie aliyeanza kufunga bao la kwanzaJerome akishangilia bao lake la kwanzaMeneja wa Noewich Alex Nail akishangilia naeNathan Redmond alipachika bao la piliWafungaji wakakutana live Nathan na JeromeWachezaji wa Boro hoi!! Mashabiki nao wakazimika!!Taswira Meneja wakiwajibika Uwanjani!Jerome alipumzishwa!

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog