Kepteni wa Liverpool Steven Gerrard amepuuza kushangiliwa na Mashabiki
wa Chelsea Jana Uwanjani Stamford Bridge walipotoka 1-1 na kuua
matumaini yao ya kufuzu 4 Bora na hivyo kukosa kucheza UEFA CHAMPIONS
LIGI Msimu ujao.
Wakati akibadilishwa katika Dakika ya 79 na kuingizwa Lukas, Gerrard alishangiliwa na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho na Mashabiki wa Chelsea na hili hasa wakitambua hiyo ni Mechi ya mwisho kwa Gerrard Uwanjani hapo kwa vile anastaafu mwishoni mwa Msimu kuichezea Liverpool.
Akiongea baada ya Mechi Gerrard alisema: "Siku zote nafurahishwa na Mashabiki wa Liverpool. Wale wa Chelsea walikuwa na heshima Sekunde chache tu na kunisakama Mechi nzima!"
Hata hivyo, Gerrard amekiri kusakamwa kwake ni kukataa kusaini kuichezea Chelsea mara 3.
Nae Mourinho alieleza: "Nimefurahishwa na kushangiliwa kwake. Nyimbo za Mashabiki wa Chelsea kumpinga ni kumtambua na kumheshimu adui yetu wa zamani tuliepigana nae muda mrefu!"

0 maoni:
Post a Comment