Sunday, May 10, 2015


Real leo hali siyo shwari!!! sare yawaangusha! Walitoka nyuma ya bao 2-0 na kusawazisha kuwa 2-2 mpaka dakika 90 zinamalizika, Ronaldo pia akikosa penati katika mtanange huo!Cristiano Ronaldo akiwa hoi baada ya kubanwa leo na Timu ya Valencia CF huku Real wakitoka Nyuma na kusawazisha bao kuwa 2-2, Sare hiyo ikiwaacha nyuma ya pointi nne dhidi ya Vinara Barcelona.

Fowadi wa Valencia CF  Paco Alcacer akishangilia bao lake la dakika ya 19

Wachezaji wa Valencia wakipongezana baada ya Javi Fuego kumfunga kipa wa Real Iker Casillas kwa mpira wa adhabu

Valencia walitangulia kipindi cha kwanza kwa kufunga bao 2-0

Ronaldo leo hoi!!  BernabeuPaco Alcacer dakika ya 19 kipindi cha kwanza anawaandikia bao la kwanza Valencia kwa kufanya 1-0 dhidi ya Real Madrid.
Pepe alianza kurudisha bao  kipindi cha pili dakika ya 56 na Isco dakika ya 84 kusawazisha bao na kufanya 2-2 na mtanange kumalizika.
Sare hii inawafanya Real kugawana pointi moja moja na Valencia huku Barcelona wakiwazidi pointi 4 Kileleni Real ambao wako nafasi ya pili. Barca wako Kileleni wakiwa na pointi zao 90 na Real wametimiza pointi 86. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Atletico de Madrid wenye pointi 76.
Valencia CF pamoja na kuwa mbele ya bao 2-0 dhidi ya Real na kulazimishwa sare wao wapo nafasi ya 4 na pointi zao 73.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog