UEFA
CHAMPIONS LIGI inarudi tena dimbani Jumanne Februari 17 kwa Mechi mbili
za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 wakati FC Shakhtar Donetsk ya Ukraine
watakapokuwa Wenyeji wa Bayern Munich na Paris Saint-Germain
kuikaribisha Chelsea ndani ya Parc des Princes Jijini Paris Nchini
France.
Jumatano Raundi ya Mtoano ya Timu 16 pia itaendelea kwa Mechi mbili ambapo Mabingwa Watetezi Real Madrid watakuwa Wageni wa Schalke huko Ujerumani.
Mechi nyingine Siku hiyo ni ile ya kule Uswisi kati ya Wenyeji FC Basel 1893 na FC Porto ya Portugal.
Mechi nyingine 4 zilizobakia za Raundi hii zitachezwa Wiki ijayo.
Msimu uliopita, Chelsea iliitoa PSG kwenye Robo Fainali za UEFA CHAMPIONS LIGI kwa faida ya Bao la Ugenini baada ya kupigwa 3-1 huko Parc des Princes katika Mechi ya Kwanza.
Mechi kati ya FC Shakhtar Donetsk na Bayern Munich huko Nchini Ukraine imehamishwa toka Mji wa Nyumbani wa FC Shakhtar, Donetsk, kwenda Lviv kwa sababu Mji huo umeshikiliwa na Wapinzani katika Vita ya wenyewe kwa wenyewe Nchini humo.
Jumatano Mabingwa Real wanacheza Nyumbani kwa Schalke ambako Msimu uliopita Uwanjani hapo hapo kwenye hatua kama hii ya Mashindano haya haya Real iliinyuka Schalke 6-1.
Msimu huu, kwenye hatua ya Makundi, Schalke pia walidundwa Bao 5-0 na Chelsea hapo hapo kwao na kupenya toka hatua hiyo baada ya kuifunga Sporting Lisbon 4-3 wakati Mabingwa Watetezi Real walivuka hatua ya Makundi kwa kushinda Mechi zao zote 6.
Katika Mechi nyingine ya Jumatano, Mabingwa wa Uswisi FC Basel, ambao waliwapiku na kuwatupa nje ya Mashindano haya Liverpool katika hatua za Makundi, wanaivaa Porto ya Ureno ambayo haikufungwa hata Mechi kwenye hatua hiyo ya Makundi.
Baadhi ya Mechi nyingine za mvuto za Wiki ijayo za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni ile ya Uwanja wa Etihad kati ya Manchester City na Barcelona hapo Februari 24 ikiwa pia ni Marudio ya Raundi kama hii ya Msimu uliopita ambayo Barcelona walishinda kwa Jumla ya Bao 4-1 katika Mechi mbili.
Siku hiyo hiyo, Mabingwa wa Italy na Vinara wa Ligi Serie A, Juventus watakuwa Wenyeji wa Borussia Dortmund iliyoanguka vibaya huko kwao kwenye Bundesliga.
Jumatano Februari 25, Arsenal ya Arsene Wenger itaivaa AS Monaco ya France ikiwa ni mara ya kwanza kwa Wenger kucheza na Klabu yake ya zamani katika Mashindano rasmi.
Mechi ya Pili ya Jumatano hiyo hiyo, ambayo itakamilisha Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ni kati ya Bayer Leverkusen na Atletico Madrid ambao ndio Washindi wa Pili wa UEFA CHAMPIONS LIGI Msimu uliopita.
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
RATIBA:
Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku leo
Jumanne 17 Februari 2015
FC Shakhtar Donetsk vs Bayern Munich
Paris Saint-Germain vs Chelsea FC
Jumatano 18 Februari 2015
Schalke 04 vs Real Madrid CF
FC Basel 1893 vs FC Porto

0 maoni:
Post a Comment