Monday, February 16, 2015


Dakika ya 88 Wayne Rooney aliipachikia bao la tatu kwa mkwaju wa penati baada ya kuangushwa ndani eneo la hatari na kipa wa Preston North End Thorsten Stuckmann kwenye Uwanja wao Deepdale Stadium, Preston  mtanange ukichezeshwa na Mwamuzi P. Dowd.Ushindi huu unawarudisha Man United Old Trafford kujiandaa na  Raundi ya 6 kuwakaribisha Wazee wa Mtutu wa London Gunners (Arsenal) Old Trafford kwenye Mchezo wa Robo Fanali katika igi hii ya FA Cup, Mtanange unaoonekana utakuwa wa kukata na Shoka siku hiyo.  

Kwa Timu ya Preston North End safari imeishia hapa na Wanajiandaa kuendelea na Ligi yao ya Championship.Dakika ya 73 Marouane Fellaini aliwapa bao la pili na kufanya 2-1 baada ya kupata krosi safi kutoka kwa Valencia na kupiga kwa kichwa langoni mwa Preston na kipa kuutema na kisha Fellaini kumalizia mpira huo lango na kufanya 2-1.
Dakika ya 65 Ander Herrera aliisawazishia bao Man united baada ya kupata pasi kutoka kwa Ashley Young aliyeingia kipindi cha pili akichukukuwa nafasi Radamel Falcao na kufanya 1-1.

Scott Laird akishangilia bao lake kwa Preston North End baada ya kufanya 1-0 dhidi ya United.Scott Laird dakika ya 47 anaipachikia bao Preston North End na kufanya 1-0 dhidi ya Manchester United akitanguliziwa  pasi na Joe Garner.

Mchezaji wa zamani wa Stevenage Laird akifurahia ushindi wa bao lake mapema kipindi cha pili huko kwenye Uwanja wao Deepdale
Laird is mobbed by his team-mates after giving the League One side a surprise lead against Premier League outfit Manchester United
Laird akiwa amezungukwa na kukumbatiwa chini na Wachezaji wenzake wa Preston baada ya kuipa bao.
Falcao akimtoka mchezaji wa Preston North End.

Marouane Fellaini akichuana na mchezaji wa Preston North End difenda Bailey Wright na kuumia pua baada ya kupigwa na kiwiko.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika Preston North End 0-0 Manchester United.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog