Friday, February 20, 2015


Mechi ya Robo Fainali ya Kombe kongwe Duniani FA CUP kati ya Timu zinazoshikilia Rekodi ya kulitwaa mara nyingi kupita wengine, Manchester United na Arsenal, imethibitishwa kuwa itachezwa Old Trafford Jijini Mnchester hapo Jumatatu Machi 9 kuanzia Saa 4 Dakika 45 Usiku, Bongo Taimu.
Man United na Arsenal kila mmoja amelitwaa Kombe hili mara 11 lakini mara ya mwisho kwa Man United kulitwaa ni Mwaka 2004 wakati Arsenal ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Msimu uliopita kufuatia kulikosa tangu Mwaka 2005.
Akiongea mara baada ya Droo ya Mechi hizi za Robo Fainali, Meneja wa Man United Louis van Gaal alisema: “Kitu muhimu ni kupangwa kucheza Nyumbani. Katika Mechi za FA CUP, naamini hilo ni muhimu, kwa hiyo nimefurahishwa tunacheza na Arsenal Nyumbani!”
Mechi nyingine za Robo Fainali ni kati ya Bradford City na Reading, Aston Villa kucheza Dabi ya Midlands na West Bromwich Albion wakati Liverpool wapo kwao Anfield kuivaa Blackburn Rovers.

FA CUP:RATIBA
ROBO FAINALI
Jumamosi Machi 7
15:45 Bradford v Reading
20:30 Aston Villa v West Brom

Jumapili Machi 8
19:00 Liverpool v Blackburn

Jumatatu Machi 9
22:45 Man United v Arsenal
TAREHE ZA RAUNDI:
-Raundi ya 6 [Robo Fainali]: 7 Machi 2015
-Nusu Fainali: 18 & 19 Aprili 2015
-Fainali: 30 Mei 2015

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog