Sunday, August 24, 2014

Wachezaji wa Everton wakipongezana baada ya kupata bao zao mbili za kipindi cha kwanza.Seamus Coleman Dakika ya 19 kipindi cha kwanza aliwapachikia Everton bao la kwanza nakufanya 1-0 dhidi ya Arsenal baada ya kulishwa mpira na Gareth Barry. 
Dakika za majeruhi za kipindi cha kwanza Steven Naismith aliwafungia bao la pili Everton na kufanya 2-0 dhidi Gunners baada ya kazi nzuri ya Romelu Lukaku kutoa pasi.
Arsenal wamefunga bao lao dakika ya 83 kupitia kwa Aaron Ramsey baada ya kupata krosi safi kutoka kwa Santi Cazorla iliyowapita mabeki wa Everton. Bao la kusawazisha Arsenal limefungwa dakika ya 90 na Olivier Giroud akisaidiwa na Monreal.
You might also like:

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog