Friday, February 14, 2014




Young Africans kesho itashuka dimbani kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya timu ya Komorozine de Domoni ya Anjuan Visiwa vya Comoro katika mchezo wa Klabu Bingwa Barani Afrika utakaofanyika mji wa Mitsamihuli kwenye uwanja wa Sheikh Said Mohamed International kuanzia majira ya 9 kamili mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
Mara baada ya jana jioni kufanya mazoezi mepesi katika uwanja mdogo wa hotel ya Retaj, leo kikosi cha Young Africans kimeweza kufanya mazoezi asubuhi majira ya saa 5 ausbuhi katika Uwanja wa Sheikh Said kwa ajili ya kuuzoea tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van der Pluijm amesema anashukuru kikosi chake kipo vizuri kuelekea mchezo huo na hakuna mchezaji majeruhi hata mmoja hivyo anapata fursa ya kuchagua amtumie nani katika mchezo huo.
Akiongelea wapinzani timu ya Komorozine de Domoni amesema hawajaidharaua mechi ya kesho kama watu wengi wanavyofikiria, kikubwa amewaandaa vijana wake waeze kufanya vizuri na kupata ushindi, "Kwangu mie hakuna mechi ndogo wala mchezo wa kirafiki" alisema Hans.
Young Africans itashuka dimbani kucheza mchezo huo wa marudiano ikiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 7-0 iliyoupata katika mchezo wa awali uliofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog