Monday, February 13, 2017


UEFA CHAMPIONS LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16 

Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku
Mechi za Kwanza
Jumanne 14 Februari 2017

Benfica v Borussia Dortmund
Paris Saint Germain v Barcelona

Jumatano 15 Februari 2017
Bayern Munich v Arsenal
Real Madrid v Napoli

Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONS LIGI, UCL, inaanza Jumanne Usiku kwa Mechi mbili na Jumatano pia zipo Mechi mbili na kuendelea Wiki ijayo, zote zikiwa ni Mechi za Kwanza za Raundi hiyo.
Jumanne ni huko Portugal wakati Benfica wakiikaribisha BVB Borussia Dortmund na nyingine ni huko Jijini Paris, Paris pale Paris Saint Germain wakicheza na Barcelona.
Jumatano pia zipo Mechi 2 za Raundi hii ambapo huko Germany ni Bayern Munich na Arsenal na nyingine ni kule Santiago Bernabeu Jijini Madrid Nchini Spain kati ya Real Madrid na Napoli ya Italy.

Mechi za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL zitakamilika Wiki ijayo, Jumanne na Jumatano kwa Mechi 4.

Dondoo Muhimu:
Benfica v Borussia Dortmund

Mechi hii itachezwa huko Estádio do Sport Lisboa e Benfica, Lisbon na kuchezeshwa na Refa mzoefu kutoka Italy Nicola Rizzoli.
Timu hizi zimekutana mara 2 Ulaya na kila moja kushinda mara moja.
Benfica watatinga kwenye Mechi hii wakiwakosa Andrija Zivkovic, alie Kifungoni, na Majeruhi Lisandro Lopez huku Jonas akiwa kwenye hatihati kucheza kutokana na maumivu.
Nao BVB watawakosa Majeruhi Mario Götze na Sven Bender huku hatihati ikiwa kwenye maumivu Nuri Şahin na Sebastian Rode.

Paris Saint Germain v Barcelona
Mechi hii ipo ndani ya Parc des Princes Jijini Paris Nchini France na itachezeshwa na Refa Szymon Marciniak kutoka Poland.

Katika Mechi zilizopita, PSG ilishinda mara 2, Sare 3 na Barca kushinda 4 kati yao.

PSG kwenye Mechi hii itamkosa Thiago Motta ambaye yupo Kifungoni wakati Barca watawakosa Majeruhi Arda Turan, Javier Mascherano na Aleix Vidal.

UEFA CHAMPIONS LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16

Mechi zote kuanza Saa 4 Dakika 45 Usiku 
Mechi za Kwanza
Jumanne 21 Februari 2017

Bayer 04 Leverkusen v Atlético Madrid
Manchester City v Monaco

Jumatano 22 Februari 2017
FC Porto v Juventus
Sevilla v Leicester City
 

Mechi za Pili
Jumanne 7 Machi 2017

Arsenal v Bayern Munich
Napoli v Real Madrid

Jumatano 8 Machi 2017

Barcelona v Paris Saint Germain
Borussia Dortmund v Benfica


Jumanne 14 Machi 2017
Juventus v FC Porto
Leicester City v Sevilla

Jumatano 15 Machi 2017
Atlético Madrid v Bayer 04 Leverkusen
Monaco v Manchester City

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog