Thursday, June 30, 2016





Afisa Mauzo (NHC), Jasson Ipyana akimuelezea mwananchi kuhusina na miradi ya nyumba ya bei nafuu ilioko nchini.
Bw: Klison Sanane (kushoto), akifafanua miradi mbalimbali ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Aika Swai (kushoto), akielezea kuhusiana na utaratibu wa unaoutumika katika ununuzi wa nyumba za (NHC) huku baadhi ya wadau kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakimsikiliza kwa umakini.
 

Banda la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) likiwa katika Maonesho ya 40 ya Kimataifa ya Biashara, yanayofanyika kila mwaka katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Sabasaba jijini Dar es salaam tayari limeanza rasmi kutoa huduma zake katika viwanja hivyo.



Afisa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Bi Edith Nguruwe akiwapa maelezo wananchi waliotembelea banda la (NHC) kuhusina na huduma zinazotolewa na Shirika hilo.



Afisa Mauzo Mwandamizi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Emmanuel Limo (kushoto), akimuelezea Wananchi Kuhusiana na mradi wa SAFARI CITY uliopo Arusha alipotembelea banda hilo katika maonesho ya Sabasaba.


Afisa biashara (NHC), Clara Lubanga akitoa ufafanuzi kwa mmoja wa Wananchi aliotembelea banda hilo kuhusiana uzwaji wa nyumba (katikati), Afisa Mauzo wa (NHC), Joseph Haule.
Serikali imesema wawekezaji wazawa wana haki ya kuwekeza kwenye sekta za mafuta na gesi ili sekta hizo ziwe na mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa nchi.Hayo yamesemwa na mtaalam kutoka Idara ya Nishati, Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi  Petro Marwa kwenye  maonesho ya  kimataifa ya  sabasaba yanayoendelea katika  viwanja  vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es  Salaam.
Mhandisi Petro alisema kumekuwepo na dhana  kuwa  wawekezaji kutoka nje ya nchi wanapewa kipaumbele katika uwekezaji kwenye gesi na mafuta  jambo ambalo si sahihi.Alisema ili kuhakikisha kuwa kila mtanzania ananufaika na uwekezaji kwenye  sekta za  gesi na mafuta,  Serikali imeweka sheria nzuri za kuwezesha watanzania kuwa sehemu  ya uchumi wa gesi na mafuta.
“ Kwa mfano Sheria ya Mafuta ya Mwaka  2015 kifungu cha  218 kinaeleza ushiriki wa serikali  kupitia Kampuni ya  Mafuta ya  Taifa (National Oil Company) na kifungu cha  219  na 220 kinaainisha ushiriki  wa watanzania katika utoaji wa  huduma na bidhaa kwa makampuni yaliyowekeza nchini kwenye  sekta za mafuta na gesi,” alisema  Mhandisi Petro.
Mhandisi Petro aliendelea kusema kuwa  serikali imeweka mikakati mbalimbali kuhakikisha watanzania wanakuwa si watazamaji  kwenye uvunaji wa rasilimali za gesi na mafuta bali wanakuwa ni washiriki kamili na kuchangia  katika ukuaji wa uchumi  wa nchi.
D1 
Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kushoto) na Mkaguzi wa Madini Mwandamizi Jeremiah Hango (kulia) kutoka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA), wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kuanza kuwahudumia wateja katika  Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
D2 
Afisa Habari, Mhandisi  Yisambi Shiwa (kulia) kutoka  Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) akielezea madini ya dhahabu yanavyochenjuliwa kwa mteja aliyeshika sampuni ya madini hayo kwenye banda la TMAA katika maonesho hayo.
D3 
Mtaalam kutoka Wizara ya Nishati na Madini, Phillip Mathayo  (kushoto) akielezea majukumu ya Wizara  kwa mteja aliyetembelea banda  hilo  katika Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
D5 
 Mmoja wa wateja (kushoto) akitoa maoni yake kwenye banda la Shirika la Madini la  Taifa (STAMICO) kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.

D7 
Neema Mwambenja kutoka Taasisi ya  Environmental Foundation for  Tanzania (EFFORT) ambayo ni mdau wa Wakala wa Nishati  Vijijini (REA) (katikati) akitoa maelezo ya shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo kwenye banda la  REA, kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Odriana Magige kutoka  taasisi hiyo.
D8 
Mhandisi Migodi kutoka Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Suleiman Khalid (katikati) akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo. Kushoto ni Afisa Usalama na Mazingira kutoka  shirika hilo Paul Thobias.
D6 
Banda la Wizara ya Nishati na Madini na Tasisi zake kama linavyoonekana pichani  kwenye kwenye Maonesho ya Kimataifa  ya Saba Saba (Dar es Salaam International  Trade  Fair)  yanayoendelea katika  Viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
———————————————
Akielezea mikakati hiyo, Mhandisi Petro alisema kuwa Serikali kupitia  Wizara ya Nishati na Madini  ilianzisha kozi mbalimbali zinazohusu mafuta na gesi katika  Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Chuo cha Madini (MRI).
Aliongeza kuwa Wizara imekuwa ikiwezesha  wanafunzi wanaofanya  vizuri katika masomo  ya sayansi kupata ufadhili wa kusomea masuala ya mafuta na gesi katika vyuo mbalimbali ndani na nje ya nchi.




Baadhi ya abiria wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo kasi maarufu kama mwendo kasi wameilalamikia kampuni hiyo kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya wizi vinavyoendelea katika baadhi ya vituo hivyo.

Bw. Juma Ally mkazi wa Kimara mwisho anasema vitendo hivyo hutokea nyakati za usiku kwa baadhi ya vijana kujifanya nao ni miongoni mwa watumiaji daraja hilo na kupelekea abiria kuibiwa vitu vyao ikiwa ni pamoja na kujeruhiwa.

Aliongezea kuwa walinzi wa kituo hicho wamekuwa wakifanya kazi ya kuwapanga abiria na kusahau majukumu yao ya kulinda usalama wa kituo hicho pamoja na mali zao.

“Tunashangaa hawa walinzi wanaolinda vituo hivi, abiria wamekuwa wakilalamika kila siku kuibiwa nyakati za usiku lakini tunaona abiria wakiendelea kuibiwa sijui wahusika wapo wapi?”Aliuliza Bw. Ally.

Nae Bi. Herrieth Shangaa aliongezea kuwa licha ya vitendo vya wizi vinavyoendelea katika vituo hivyo kuna baadhi ya vitendo vikiwemo vya kujisaidia katika madaraja hayo hivyo kupelekea uchafuzi wa mazingira

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi msimamizi wa vituo hivyo ambae hakutaja kutajwa jina lake amesema kuna baadhi ya vituo ni vikubwa na wanawalinzi wachache hivyo wamejipanga kuongeza ulinzi ikiwa ni pamoja na kufunga mfumo wa kidigitali wa kudhibiti wahalifu

Mradi wa mabasi yaendayo haraka ulioanza rasmi terehe 10, mei, 2016 umeonesha ni jinsi gani kero ya foleni itakavyopungua kwa kuwa mabasi hayo yanatumia njia yake ambayo ni miundombinu iliyojengwa kwa gharama kubwa sana.

Mbunge wa Ubungo Chadema Saed Kubenea amesimamishwa kuhudhuria vikao vitano vya bunge na Naibu Spika Dk Tulia Akson baada ya kubainika kusema uongo kwamba Waziri wa Ulinzi na JKT Dk Hussein Mwinyi ameingia Mkataba na kampuni ya China Henan International Cooperation Group Company wa ujenzi wa nyumba za JWTZ na nyumba ya Waziri huyo jambo ambalo sio kweli.
Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi amesimamishwa kuhudhuria vikao kumi vya bunge kuanzia leo June 30 mwaka huu baada ya kubainika kunyosha kidole cha kati kwa wabunge baada ya kukiri mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka kwamba alifanya kitendo hicho. Hata baada ya kuhojiwa Mbunge Mbilinyi alishindwa kumtaja Mbunge wa CCM aliyedaiwa kumtukana ili nae achukuliwe hatua na kamati hiyo. Bunge limeridhia adhabu hiyo iliyotolewa na kamati.

KONGAMANO kubwa la aina yake limefanyika mjini Dar es salaam ambapo washiriki walizungumzia namna ya kuendeleza rasilimali watu katika eneo la utaalamu na taaluma katika shughuli mbalimbali za uendelezaji wa makampuni na viwanda.

Kongamano hilo ambalo lilihudhuria na watu wenye kariba kubwa katika masuala ya viwanda na biashara akiwemo Dkt. Reginald Mengi ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF);na Balozi wa Ufaransa nchini Malika Berak liliangalia uhaba wa wataalamu na namna ya kuuondoa uhaba huo wakati taifa linaelekea katika uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Wengine waliokuwepo katika kongamano hilo Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero na maofisa wa serikali.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akikaribisha washiriki na wadau wengine alisema kwamba mafunzo hayo yaliyoratibiwa kwa pamoja katika wataalamu wa Ufaransa, ESRF na Benki ya Maendeleo ya Afrika yamelenga kudadavua tatizo lililopo na kulipatia ufumbuzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) akisalimiana na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) alipowasili katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak.(Picha na Modewjiblog)

Taasisi ya utoaji mafunzo ya Ufaransa ya AFPA ndiyo ilikuwa inaendesha mafunzo hayo wakibadilishana uzoefu na wadau wa Tanzania kutoka sekta binafsi.

Akifafanua zaidi Dkt. Kida alisema kwamba kongamano hilo limelenga zaidi katika kubadilishana uzoefu kuhusu changamoto zinazojitokeza na fursa zilizopo katika mafunzo, ukuzaji na uendelezaji taaluma.

Dkt. Kida alifurahishwa na mchanganyiko wa watu kutoka sekta binafsi waliofika katika kongamano hilo ambao aliamini kwamba wataelezea uzoefu wao katika kukabiliana na changamoto za taaluma katika makampuni yao.

Aidha alisema kwamba wadau hao wa Tanzania watapata uzoefu wa timu ya wataalamu wanne kutoka kwa wakala wa mafunzo ya taaluma nchini Ufaransa (AFPA) ambao wataeleza miaka 60 ya uzoefu katika masuala ya mafunzo ya taaluma na uendelezaji wa utaalamu.

Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak (kushoto) akibadilishana mawazo na mgeni rasmi Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi (TPSF), Dk. Reginald Mengi (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida katika ofisi za ESRF jijini Dar es Salaam.

Alisema anaamini kwamba mchanganyiko huo wa wadau utasaidia katika kukabiliana na tatizo la taaluma katika soko la ajira la Tanzania.

Alisema mazungumzo hayo ni muhimu sana katika kuibua fursa hasa wakati taifa hili linajipanga kuelekea katika uchumi wa kati wa viwanda na bila wataalamu wenye taaluma zao makamapuni na viwanda vingi vitakuwa na shida kubwa.

Alisema changamoto kubwa inayokabili taifa la Tanzania kuelekea nchi ya viwanda kama ilivyo katika nchi nyingine zinazoendelea ni ukosefu wa taaluma na utaalamu.

“Ukosefu wa wafanyakazi wenye taaluma katika ngazi zote ni tatizo kubwa linalokabili harakati za kuelekea uchumi wa viwanda” alisema Dkt. Kida.

Anasema pamoja na matatizo hayo taasisi yake tayari imeshaanza kushughulikia shida hiyo ya taaluma nchini Tanzania kwa kuwa na makongamano mbalimbali makubwa yanayokutanisha wadau kuzungumzia hali hiyo.
Balozi wa Ufaransa nchini, Mh. Malika Berak (kulia) akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero (kushoto) alipowasili ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida (katikati) kabla ya kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano.

Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na mke wa tajiri namba moja duniani na mwenyekiti mwenza wa Bill and Melinda Gates Foundation, Melinda Gates kwa pamoja wamelipongeza Shirika la Oxfam kupitia kampeni yake ya Grow kwa kufanya Shindano la Mama Shujaa wa Chakula kama moja ya mbinu za kumkomboa mwanamke mnyonge kiuchumi.

Wawili hao waliyasema hayo kwenye mdahalo uliofanyika Juni 29 mwaka huu katika bustani ya Hoteli ya Serena jijini Dar ambapo walikuwa wageni waalikwa waliopata fursa ya kuzungumzia jinsi ya kumuwezesha kiuchumi mwanamke mzalishaji na namna ya kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Akizungumza kwenye mdahalo huo, Melinda Gates alisema kuwa yeye kupitia Bill and Melinda Gates Foundation wamelenga kusaidia nchi nyingi hasa za ukanda wa Afrika Mashariki kama Tanzania katika kubadilisha maisha yao kwa kutengeneza fursa za ajira na kuwasaidia vitendea kazi. 

Aliongeza kuwa kwa nchi kama ya Tanzania ambayo asilimia 25 ya mapato yake yanatokana na kilimo, taasisi yao imejikita katika kuwawezesha wakulima wadogowadogo ambao hata hivyo huwezi kuwaacha wakina mama kwa kuwa ndiyo wanaotoa mchango mkubwa kwenye sekta hiyo. 

Akizungumzia kuhusu Shindano la Mama Shujaa wa Chakula, Melinda Gates alitoa pongezi zake za dhati kwa shirika la Oxfam na kuongeza kuwa, ikiwa nchi za Kiafrika hususan Tanzania itataka kupiga hatua lazima iwawezeshe kiuchumi wanawake kwa kuwa wao ndiyo wenye uwezo wa kubadilisha maisha yao na hilo ndiyo jambo muhimu zaidi. 

Naye Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye mdahalo huo alisema kuwa; kwa kipindi kirefu amekuwa mfuatiliaji wa mashindano hayo na kuahidi kuwa sera ya serikali ya awamu ya tano ni kuongeza vipaumbele kwa mwanamke kwa kutoa mianya kwa taasisi zinazomsaidia mwanamke ikiwemo shirika la Oxfam kupitia shughuli zake hasas shindano la mama shujaa wa chakula. “Nikiri tu kuwa nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa shindano hili tangu zamani, naahidi kuwapa ushirikiano mkubwa kwenu kwa kila jambo kwa kuwa mnaisaidia sana serikali,” alisema Ummy. 

Aidha mdahalo huo pia ulioongozwa na mwanaharakati, Maria Sarungi Tsehai ulihudhuriwa na wanaharakati wengine wa masuala ya jinsia akiwemo Mkurugenzi wa Msichana Initative, Rebecca Gyumi, Mwanaharakati wa Mtandao wa Masuala ya Kijinsia, Marjorie Mbilinyi, Mwezeshaji kutoka Forum CC, Faizal Issa na Mshindi wa Shindano la Mama Shujaa wa Chakula 2011, Anna Oloishuro.

Mwenyekiti mwenza wa taasisi ya Bill and Melinda Gates ya Marekani Bi. Melinda Gates akiongea na wadau mbalimbali na kulipongeza shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo lengo kubwa ni kuwawezesha wakulima wadogo wadogo wanawake kufanikiwa katika Kilimo cha chakula na umiliki wa ardhi.
Mkurugenzi Mkazi wa Oxfam Tanzania Jane Foster akitoa neno la utangulizi wakati wa sherehe hiyo.
Waziri wa Afya,Jinsia,Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu akilipongeza Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania kwa kuendesha Shindano la Mama Shujaa wa Chakula ambalo linaonesha changamoto za wazalishaji wa chakula wadogo ikiwemo umiliki wa ardhi.
Mshereheshaji katika Hafla hiyo Maria Sarungi Tsehai akiendelea kutoa muongozo


Wateja wakipata maelezo kuhusu huduma za TTCL, katika viwanja vya sabasaba
 Afisa kutoka TTCL, Fredrick Benard (kushoto) akitoa maelezo kwa mteja aliyetembelea banda la TTCL.

 TTCL wakitoa huduma kwa wateja katika maonesho ya Sabasaba 
 Wafanyakazi wa TTCL wakitoa huduma kwa wateja.
 Wafanyakazi wa TTCL wakiwakaribisha wateja katika Banda.

Wananchi waendelea kujitokeza kwa wingi katika Banda la Kampuni ya Simu Tanzania(TTCL) kununua bidhaa bora za  4G katika viwanja vya Maonesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya Sabasaba. 

Akizungumza katika Maonesho hayo, Emerco Mashele Afisa kutoka TTCL amesema kuwa katika msimu huu wa Maonesho ya Kimataifa ya SabaSaba, kampuni imeendelea kuwaletea watanzania bidhaa nzuri za 4G – LTE, zenye kiwango kikubwa cha ubora, bei nafuu na uhakika. 

“Safari hii tumewaletea Wananchi bidhaa bora na nzuri katika matumizi ya mawasiliano ya simu. Kwa huduma zetu tunatoa fursa kwa wateja wetu kupata intaneti yenye kasi ya 4G ukiwa na Laini za 4G ambazo zinapatikana hapa katika Banda TTCL na ofisi za TTCL katika jiji la Dar es salaam” amesema Emerco. 

Aidha, Bw. Emerco aliongeza kuwa katika Maonesho haya ya SabaSaba, TTCL inatoa fursa ya wananchi kupata   laini ya 4G, Modemu ya 4G, Mi-Fi ya 4G na Routers ya 4G.

Katika maonesho haya tuna laini za 4G ambazo zinapatika hapa na katika ofisi zetu za TTCL, Mteja anaweza kifaa cha 4G Mi-Fi ambapo mteja anaweza kuunganisha watu wengine 10 na kupata intaneti katika ubora ule ule. 4G Routers inauwezo wa kuunganisha watu 32 na inauwezo kwenda katika ubora ule ule, Aidha pia Routers inatoa fursa kwa watumiaji kupata huduma simu ya Mezani.


 Na Mwene Said wa Globu ya Jamii, Dar es Salaam
Tundu Lissu (48) amesomewa mashtaka ya kutoa lugha ya uchochezi ikiwemo kudharaulisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lissu alisomewa mashtaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Juni 30, 2016.

Upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu Bernad Kongola akisaidiana na Mawakili wa Serikali Waandamizi, Nassoro Katuga na Salum Mohammed.

Kongola alidai kuwa Juni 28,2016 eneo la Mahakama ya Kisutu Ilala Dar es Salaam mshtakiwa kwa nia ya kushawishi na kudharaurisha watanzania dhidi ya mamlaka halali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alinukuu maneno ya Lissu kwamba"Mamlaka ya Serikali mbovu ya kidikteta uchwara inahitaji kupingwa na kila mtanzania kwa nguvu zote, huyu dikteta uchwara lazima apingwe kila sehemu kama uongozi utafanywa na utawala wa kijinga nchi inaingia  ndani ya giza nene"

Mshtakiwa alikana mashtaka hayo.

upande wa jamhuri ulidai upelelezi umekamilika na uliomba tarehe ya kusikilizwa maelezo ya awali.
Upande wa utetezi ukiongozwa na jopo la mawakili 11 akiwemo Michael Ngalo, Peter Kibatala na wenzao uliomba dhamana kwa mshtakiwa kwa kuwa ni mbunge atakuwa mwaminifu hataacha kufika mahakamani.

Hakimu Yongolo alisema mshtakiwa atakua nje kwa dhamana kwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana ya sh milini 2.

alitimiza masharti atasomewa maelezo ya awali Agosti 2,2016.

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa kutumia au kwa kutotumia mawakala.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Amesema katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali. “Moja ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala au Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash transactions),” alisema.

Amesema katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.

Amesema Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Sheria hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato, na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.

Amesema hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

“Pamoja na dhamira nzuri ya hatua hizo, tunayo mifano ya baadhi ya Halmashauri kama vile Nzega ambayo baadhi ya wahusika wameshinikiza wakitaka zabuni zote wapewe madiwani. Jambo hili halikubaliki na tena ni kinyume cha maadili ya utumishi,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kwamba kuanzia Julai Mosi, 2016 zihakikishe zinatumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato, katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya kuboresha makusanyo iwe yanakusanywa na Halmashauri au na wakala.

Amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya Serikali pamoja na michango ya wananchi licha ya kuwa uzoefu unaonesha kuwa mamlaka hizo zina tatizo la kukaa na fedha kwa muda mrefu kabla ya kuzielekeza kwenye matumizi yaliyokusudiwa.

“Kuchelewesha kutoa fedha zilizotengwa kwa shughuli zilizopangwa ni kuchelewesha kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Napenda kuhimiza uzingatiaji wa utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya fedha za Serikali katika ngazi zote ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya umma,” aliongeza.

Mkutano huo wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19, 2016 ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 6, mwaka huu litakapokutana tena mjini Dodoma.



Meneja wa kituo cha kusimamia wasanii ‘Mkubwa na Wanae’ Said Fella ameelezea ndani ya miaka mitano kituo chake kimefanya kitu gani kwenye tasnia ya Bongo Fleva na mabadiliko yaliyoonekana.
Mpaka sasa hivi Mkubwa na wanae ina miaka mitano na kuna vitu vingi vilivyofanyika na watu wanaona,  nimekuwa na kituo ambacho kinakuza wasanii na watu wananipa hongera, kikubwa kwenye suala la kukusanya wasanii mpaka kuwaongeza lazima kutakuwa na changamoto cha msingi kujua wapi pa kuanzia na pa kuelekea’- Mkubwa Fella

Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba leo June 30 imetangaza rasmi kupitia kurasa zake za mitrandao ya kijamii kuingia mkataba na kocha raia wa Cameroon Joseph Omog, Simba wametangaza kuingia mkataba na Omog bila kuweka wazi mambo kadhaa kwa kigezo kuwa taarifa rasmi itatoka kesho July 1.
Simba wameingia mkataba na Omog ambaye amewahi kuifundisha klabu ya Azam FC na kuipatia Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2013/2014 kwa mara ya kwanza, Omog kwa sasa ana umri wa miaka 44 na anatajwa kuwa kesho ndio atatambulishwa rasmi kujiunga na Simba.
mnnn
Rapper kutoka Bongoflevani, Darasa anayetamba na wimbo uitwao Kama  Utanipenda aliyomshirikisha Rich Mavoko , sasa leo June 30, 2016 alikutana na waandishi wa habari kwaajili ya kuzinduzi single yake mpya iitwayo Too Much.
Wimbo huo mpya umeandaliwa kwenye kipindi cha miezi sita iliyopita kupitia studio ya Mr. T Touch na kwenye upande wa video mikono ya director Hanscana imehusika.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari alisema…’Kila iitwayo leo katika kazi zangu nikiifanya bora zaidi ya jana nashukuru watanzania wamenielewa kazi zangu, sasa leo niwaletea kitu kipya cha ‘Too Much’ ambacho nimefanyia hapa bongo, nimefanikiwa kuufanya muziki wangu kuwa wa tofauti katika ladhaa zake, mtihani wangu ndiyo huu kwa shabiki’Darasa


ENGLAND inatafakari uwezekano wa kumteua Gareth Southgate awe Meneja wa Muda wa England kufuatia kuondoka kwa Roy Hodgson mara baada ya England kutupwa nje ya EURO 2016 kwenye Hatua ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Iceland huko France.
Southgate, ambae sasa ndie Bosi wa Timu ya Taifa ya England ya Vijana chini ya Miaka 21, U-21, anaweza kuteuliwa ili kuisimamia Timu hiyo ikianza kampeni yake ili kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Wakiongea na Wanahabari, Mtendaji Mkuu wa FA, Chama cha Soka England, Martin Glenn, akiwa pamoja na Roy Hodgson hapo Jana, alidokeza kuwa kumsaka Meneja mpya kunaweza kuchukua Miezi kadhaa.

Hivi sasa huko England Majina kadhaa yamekuwa yakitajwatajwa n ahata Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambae sasa yuko kwenye Mwaka wa mwisho wa Mkataba wake na Arsenal, anatajwa mno kufaa kuwa Meneja mpya wa England.

Alipoulizwa moja kwa moja kama Southgate anaweza kuiongoza Timu kwa ajili ya Mechi yao ya kwanza ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za 2018 hapo Septemba dhidi ya Slovakia, Glenn alijibu: “Tutaona. Tunataka tumpate kabla ya hiyo michujo ya Kombe la Dunia lakini kama hatukumpata tuna mipango ya muda. Hatuzungumzii Majina lakini hilo lake lipo wazi!”

Mchakato wa kumpata Meneja mpya wa England utasimamiwa na Glenn mwenyewe pamoja na Mjumbe wa Bodi ya FA, David Gill, na Mkurugenzi wa Ufundi wa FA, Dan Ashworth.

Wednesday, June 29, 2016

Mkali wa Bongo fleva, Harmonize ambaye ni msanii wa kwanza kusainiwa kwenye lebo ya Diamond Platnumz (WCB), amekaa kwenye interview hii na Millard Ayo na amezungumzia kuhusu kujiendeleza zaidi katika masuala ya lugha, Harmonize amesema…
>>>’Kuna mwalimu pale ofisini WCB anafundisha lugha lakini kuiongea lugha kabla haujaijua vizuri si kitu kizuri kiiungwana, kuna mwalimu pale special kabisa  kwa sababu msanii yoyote wa WCB kwa sababu tunahitaji kutanua mziki wetu ufike tuwe na market ya nje pia’
>>>’hatuwezi kuwa na biashara ya nje, unawezaje kuwa na biashara nje na wakati international language hauwezi kuiongea, inakuwa ni vigumu kwa hiyo tunajaribu na management ililiona hilo mapema na likaishughulikia kuna mwalimu pale anatufundisha lugha vizuri tu‘- Harmonize


Liverpool wamekamilisha kumsaini Sadio Mane kwa Dau la Pauni Milioni 34 kutoka Southampton na kumpa Mkataba wa Miaka Mitano.
Dau hilo linaweza kupanda na kufikia Pauni Milioni 36 likizidi lile la Mchezaji alienunuliwa na Liverpool kwa ghali kupita yeyote walipotoa Pauni Milioni 35 kumnunua Andy Carroll Mwaka 2011.
Dili hii imemfanya Mane, anaetoka Senegal, kuwa ndie Mchezaji wa Bei ghali kupita yeyote katika Historia akilipiku lile la Januari 2015 ambalo Man City walilipa Pauni Milioni 28 kwa Swansea City kumnunua Wilfried Bony.

Mane, ambae alifunga Bao 21 katika Gemu 67 za Ligi Kuu England alizochezea Southampton tangu ahamia hapo kutoka Salzburg Mwaka 2014, anakuwa Mchezaji wa Tatu kusainiwa na Meneja Jurgen Klopp katika kipindi kufuatia Kipa wa Germany Loris Karius na Beki wa Cameroon Joel Matip. Mane anafuata mlolongo wa Wachezaji kadhaa wa Southampton walionunuliwa na Liverpool tangu 2014 na wengine ni Adam Lallana, Dejan Lovren, Rickie Lambert na Nathaniel Clyne.
Leo June 29 2016 Mahakama Kuu Kanda ya Arusha imetengua matokeo ya ushindi yaliyompa Ubunge, Onesmo Nangole ‘CHADEMA’  jimbo la Longido kutokana na udanganyifu.
Akisikiliza kesi hiyo Jaji Sivangilwa Mwangesi amesema fomu zilizotumika kuandika matokeo ni fomu 21b za udiwani badala ya kutumia fomu 21c za ubunge hivyo uchaguzi utarudiwa.
Kesi hiyo ilifunguliwa mnamo June 29 2016 mahakama kuu Arusha na aliyekuwa mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi ‘CCM’ jimbo la Longido Dk. Steven Kiruswa.
Baada ya ushindi wa kesi hiyo dhidi ya Onesmo Nangole ‘CHADEMA’ Dk. Kiruswa ‘CCM’ amesema…..>>>’tunangojea wenzetu kama wana sababu ya kukata rufaa, wakate baada ya hapo tutaenda uwanjani kuanza upya….tulikuwa na madai mengi ya msingi lakini moja ni kuwepo kwa kasoro katika utaratibu waliotumia kuhesabu, kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi

June 28 2016 ziliripotiwa taarifa kuwa watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalamu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium nchini Tanzania.
Leo June 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli kupitia account yake ya tweeter amepost akizungumzia ugunduzi huo huku akitoa wito kujipanga katika eneo la mikataba…….



Imeripotiwa kuwa watu 36 wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Ataturk Istanbul nchini Uturuki na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa, shughuli za usafirishaji katika uwanja huo zimesitishwa huku shughuli ya uokoaji na huduma ya kwanza vikiendelea.
Gavana wa mji wa Istanbul amethibisha kuuawa watu haona idadi hiyo ya majeruhi. Mashuhuda wanasema waliwaona washambuliaji watatu ambapo mmoja kati yao alikuwa akifyatua risasi kabla ya kujitoa muhanga kwa kujilipua kwa bomu na kufa.
DM GRAB - Ataturk Airport International Terminal terrorists images appeared on the departures floor. Images of the Russian national airline Aeroflot experienced moments of horror in front of the bank where the check-in office and this was reflected in the cameras. (Haberturk News Centre)
Hata hivyo mashambulizi hayo yalihusisha katika eneo la kuingia katika uwanja huo. Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amelaani shambulio hilo na kusisitiza umoja katika kutokomeza vitendo hivyo.
.
.
.
.
.
.
.n
.n
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.

waliotembelea blog