Saturday, December 24, 2016


MABINGWA watetezi Tanzania bara Yanga wamelazimishwa sare ya bao 1-1 katika mchezo wa 17 wa Ligi Kuu Soka Tanzania bara dhidi ya African Lyon.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, mabao yalifungwa na Ludovick Venance wa African Lyon na Amis Tambwe kwa upande wa Yanga.
Sare hiyo itaendelea kuibakiza Yanga kwenye nafasi ya pili ikifikisha jumla ya pointi 37 nyuma ya vinara Simba yenye pointi 38.
Matokeo hayo yana faida kwa Simba kama itashinda mchezo wake wa leo dhidi ya JKT Ruvu utakaochezwa kwenye uwanja wa Uhuru, itawaacha wapinzani wake kwa tofauti ya pointi nne kwa kuwa itafikisha pointi 41.
Hata kama Simba itafungwa au kupata sare yoyote bado itaendelea kuongoza.
African Lyon ndio ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika 59 lililofungwa na Venance baada ya kupata krosi nzuri ya Abdallah Mguhi.
Venance aliingia kipindi cha pili dakika 46 kuchukua nafasi ya Awadh Juma.
Aidha, Tambwe akaisawazishia Yanga dakika ya 74 kwa kichwa baada ya kupata krosi ya Juma Abdul.
Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kila timu haikuweza kufumumania nyavu ya mwenzake.

Yanga ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga na kushindwa kuzitumia kupitia kwa Tambwe, Haruna Niyonzima, Vicent Bossou, Thaban Kamusoko, Simon Msuva na Geofrey Mwashiuya huku Mguhi kwa upande wa African Lyon akikosa pia.
African Lyon inapata sare ya pili mfululizo na kufikisha pointi 19. Timu hii inazidi kujiwekea rekodi kwa kuzibana timu tatu zinazoongoza ligi, ikitoka kuilazimisha Azam FC sare ya bila kufungana na pia, iliifunga Simba bao 1-0 katika mchezo wa raundi ya kwanza.

Kikosi cha Yanga kilikuwa na Deogratius Munishi 'Dida', Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, Saidi Juma, Simoni Msuva, Thabani Kamusoko/Obrey Chirwa, Amisi Tambwe, Haruna Niyonzima na Deusi Kaseke/Emmanuel Martin.
African Lyon; Jehu Youthe, Miraj Adam, Baraka Jaffary, Halfan Twenye, Hamadi Waziri, Hamadi Manzi, Hassan Isihaka, Omary Abdallah, Awadh Juma/Ludovick Venance, Thomas Maurice na Abdallah Mguhi.


Mechi 14 za Ligi Kuu ya Vodacom zinatarajiwa kufanyika wakati huu wa msimu wa kufunga mwaka 2016 na mbili za zitafungua mwaka 2017 ambako Kituo cha Televisheni cha Azam - Wadhamini wenza wa ligi hiyo, wamethibitishia Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupata burudani kwa michezo yote kulingana na ratiba.

Katika Ligi hiyo ambayo pia inabarikiwa na Benki ya Diamond Trust (DTB), michezo 15 ya kipindi cha sikukuu za kufunga na kufungua mwaka inatarajiwa kuanza saa 10.00 jioni isipokuwa ule wa Mbao FC na Mwadui uliopangwa kuanza saa 8.00 mchana kama itakavyojieleza hapo chini kwenye mtiririko wa ratiba.

Burudani kwa Wote katika michezo hiyo kutoka Azam Tv, zinaanzia mchezo wa kesho Ijumaa wa Desemba 23, mwaka huu ulipewa jina la Na. 129 utakaozikutanisha timu za African Lyon na Young Africans kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Kamishna wa mchezo anatarajiwa kuwa Idelfonce Magali kutoka Morogoro.

Katika mchezo huo unaotarajiwa kuchezeshwa na Mwamuzi, Ludovic Charles kutoka mkoani Tabora akisaidiwa na John Kanyenye wa Mbeya (Mshika Kibendera Na. 1) na Alnord Bugado wa Singida (Mshika Kibendera Na. 2), Mwamuzi wa Akiba – Mezani anatarajiwa kuwa Israel Nkongo kutoka Dar es Salaam.
Jumamosi Desemba 24, 2016 kutakuwa na mechi sita ukianzia ule wa Mbeya City na Toto Africans zitacheza kwenye Uwanja wa Sokoine jijiji Mbeya katika mchezo Na. 130 utakaosimamiwa na Kamishna George Komba wa Dodoma wakati Mwamzi wa kati atakuwa Shakaile ole Shangalai wa Pwani huku wasaidizi wake wakiwa ni Khalfan Sika pia wa Pwani na Vecent Milabu wa Morogoro. Mwamuzi wa akiba atakuwa Cherles Mwamlima.

Mchezo Na. 131 utazikutanisha timu za Kagera Sugar na Stand United katika Uwanja wa Kaitaba, uliko Kagera ambako utasimamiwa na Kamishna Nassoroi Hamduni wa Kigoma huku Mwamuzi akiwa ni Jacob Adongo wa Mara akisaidiwa na Joseph Masija na Robert Luhemeja kutoka Mwanza na Mezani atakuwa Jonesia Rukyaa wa Kagera.

Ndanda itaendelea kubaki nyumbani kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara na baada ya kucheza na Simba juma lililopita na kupoteza mchezo huo, safari hii inaikaribisha Mtibwa Sugar ya Morogoro katika mchezo Na. 132 utakaosimamiwa na Kamishna Jimmy Lengwe wa Morogoro wakati Mwamuzi atakuwa Andrew Shamba wa Pwani akisaidiwa na Haji Mwalukuta wa Tanga na Jeremiah Simon wa Dar es Salaam. Mezani atakuwa Abubakar Mtulo.

Siku hiyo pia kutakuwa na mchezo kati ya Simba na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mchezo huo Na. 133 utafanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ambako utasimamiwa na Tito Haule wa Morogoro na kuchezeshwa na Mwamuzi Hans Mabena wa Tanga. Mabena atasaidiwa na Omari Kambangwa wa Dar es Salaam na Khalfan Sika wa Pwani wakati Mbaraka Rashid wa Dar es Salaam atakuwa Mwamuzi wa Akiba – mezani.

Baada ya kulala Mbeya mbele ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Sokoine, Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Azam FC ya Dar es Salaam ambayo juma lililopita iliambulia sare tasa kutoka kwa African Lyon. Majimaji na Azam zinakutana kwenye mchezo Na. 134 utakaofanyika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.

Katika mchezo huo ambao Mwamuzi atakuwa Ngole Mwangole wa Mbeya ambaye ni mwamuzi bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita, atasaidiwa na Mirambo Tshikungu na Mashaka Mwandembwa – pia wote wa Mbeya huku kamishna akiwa ni David Lugenge wa Iringa.

Mwadui ambayo ilianza vibaya duru la pili kwa kupoteza mchezo uliopita, Jumamosi Desemba 24, mwaka huu itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Mwadui Complex mkoani Shinyanga. Mchezo huo Na. 135, utasimamiwa na Kamishna Staricko Nyikwa wa Singida katika mchezo utakaoanza saa 8.00 mchana ili kutoa fursa kwa mdhamini Azam kuonesha mchezo huo moja kwa moja ikiwa na maana ya mubashara.

Waamuzi wataongozwa na Emmanuel Mwandembwa atakayesimama katikati kupuliza filimbi huku akisaidiwa na Abdallah Uhako na Agnes Pantaleo wote wa Arusha na mezani anatarajiwa kuwa Ezekiel Mboi wa Shinyanga.

Krismas, yaani Desemba 25, 2016 hakutakuwa na mchezo ila siku inayofuata Desemba 26, mwaka huu Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Mabatini, ulioko Mlandizi mkoani Pwani katika mchezo Na 136.

Manyama Bwire wa Dar es Salaam atakuwa Kamishna wa mchezo huo wakati Mwamuzi ni Forentina Zabron wa Dodoma akisaidiwa na Hassan Zani wa Arusha na Silvester Mwanga wa Kilimanjaro. Mwamuzi wa akiba - Mezani atakuwa Andrew Shamba wa Pwani.

Desemba 28, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili ambako Young Africans ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru jijini katika mchezo Na. 137 ambako Juma Chiponda wa Tanga atakuwa kamishna wa mchezo huo.

Mwamuzi wa kati katika mchezo huo atakuwa Eric Onoca wa Arusha akisaidiwa na Michael Mkongwa wa Njombe na Janeth Balama wa Iringa. Mwamuzi wa akiba atakayekaa mezani atakuwa Mwanahamisi Matiku wa Dar es Salaam.

Kadhalika siku hiyo, Majimaji ya Songea itakuwa mgeni wa Mtibwa Sugar ya Morogoro kwenye Uwanja wa Manungu ulioko Mvomero katika mchezo Na. 138 utakaosimamiwa na Kamishna Pius Mashera wa Dodoma, utachezeshwa na Mathew Akrama kutoka Mwanza akisaidiwa na Abdallah Rashid wa Pwani na Gasper Ketto wa Arusha. Mwamuzi wa akiba atakuwa Selemani Kinugani.

Kadhalika Desemba 29, mwaka huu kutakuwa na mechi mbili. Ruvu Shooting ya Pwani inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba ya Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam katika mchezo ambao mwamuzi atakuwa Alex Mahagi wa Mwanza.
Katika mchezo huo Na. 139, Mahagi atasaidiwa na Ferdinand Chacha pia wa Mwanza na Rashid Zongo wa Iringa huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hellen Mduma wa Dar es Salaam. Kamishna wa mchezo atakuwa Peter Temu wa Arusha.

Azam ya Dar es Salaam itatulia nyumbani Uwanja wa Azam huko Chamazi ikicheza na Tanzania Prisons ya Mbeya katika mchezo Na. 140 utakaosimamiwa na Elizabeth Kalinga wa Mbeya huku Mwamuzi akiwa ni Jimmy Fanuel wa Shinyanga huku wasaidizi wake wakiwa ni Makame Mdog pia wa Shinyanga na Abdallah Mkomwa wa Pwani huku Kassim Mpinga akiwa ni mwamuzi wa akiba.

Saa kadhaa kabla ya kuingia mwaka 2017, yaani Desemba 31, mwaka huu kutakuwa na michezo miwili ambako Mwadui ya Shinyanga itacheza na Kagera Sugar ya Kagera kwenye Uwanja wa Mwadui mkoani Shinyanga katika mchezo Na. 141.

Kamishna anatarajiwa kuwa Nassib Mabrouk wa Mwanza na Mwamuzi ni Isihaka Mwalile na wasaidizi wake ni Hellen Mduma na Omary Kambangwa – wote kutoka Dar es Salaam. Julius Kasitu wa Shinyanga anatarajiwa kuwa Mwamuzi wa Akiba.
Kadhalika siku ya funga mwaka, Mbeya City inatarajiwa kucheza na Mbao FC kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya katika Mchezo Na. 143 ambao msimamizi wa mchezo atakuwa Joseph Mapunda wa Ruvuma.

Mwamuzi katika mechi hiyo anatarajiwa kuwa Hussein Athuman wa Katavi wakati wasaidizi wake watakuwa ni Lulu Mushi wa Dar es Salaam na Nicholaus Makaranga wa Morogoro. Mwamuzi wa Akiba Mezani atakuwa Mashaka Mwandembwa wa Mbeya.

Januari mosi kutakuwa na michezo miwili tu ya kukaribisha Mwaka Mpya ambako Toto African ya Mwanza itacheza na Stand United ya Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo Na. 144 utakaosimamiwa na Jovin Bagenda wa Kagera. Mwamuzi atakuwa Israel Nkongo sambamba na wasaidizi wake Soud Lila na Frank Komba, wote wa Dar es Salaam. Mwamuzi wa akiba mezani atakuwa Mathew Akrama wa Mwanza.
Pia African Lyon ya Dar es Salaam itakuwa mwenyeji wa JKT Ruvu katika mchezo Na. 142 utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kamishna atakuwa Hamisi Kitila wa Singida wakati Mwamuzi anatarajiwa kuwa Selemani Kinugani wa Morogoro wakati wasaidizi wake ni Omary Juma wa Dodoma na Agnes Pantaleo wa Arusha wakati mezani atakuwa Shafii Mohammed wa Dar es Salaam.

Mara baada ya michezo hiyo, Ligi Kuu ya Vodacom itasimama kwa wiki mbili kupisha michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Januari mosi, mwaka huu.

Thursday, December 22, 2016


FIFA Leo hii imetoa Listi ya Ubora Duniani ambayo ni ya mwisho kwa Mwaka 2016 na Argentina wameendelea kushika Nambari 1 wakifuata Brazil.
Tanzania imepanda Nafasi 4 na sasa ipo ya 156 kutoka ile ya 160 ya Mwezi uliopita.
Mwezi Januari Mwaka huu Tanzania ilikuwa ya 126 na kupanda hadi 125 Mwezi Februari, kushuka 130 Aprili na kuyumba lakini Julai ikawa ya 123 na baada ya hapo mporomoko ukafuatia.

Kwa Bara la Afrika, Timu inayoshika Nafasi ya juu kabisa ni Senegal ambao ni wa 33 wakifuata Mabingwa wa Afrika Ivory Coast walio Nafasi ya 34 kisha Tunisia 35, Egypt 36 na Algeria 38.

10 BORA:
1. Argentina
2. Brazil
3. Germany
4. Chile
5. Belgium
6. Colombia
7. France
8. Portugal
9. Uruguay
10. Spain


KIUNGO wa Manchester United Henrikh Mkhitaryan Leo amezoa Tuzo yake ya 6 mfululizo kama Mchezaji Bora wa Mwaka kwa Nchi yake Armenia.
Hii ni Tuzo yake ya 7 tangu avuke Umri wa Miaka 20 na kumfanya awemo kwenye Rekodi za Mastaa wa Dunia waliozoa mara nyingi Tuzo za aina hiyo.
Anaeongoza kwa Tuzo aina hii kwa Nchi yake ni Mchezaji mwenzake Mkhitaryan huko Man United, Zlatan Ibrahimovic, ambae amechukua mara 11.
Wengine wanaomkimbiza Ibrahimovic ni Wachezaji toka Finland, Sami Hyypia, alietwaa mara 9 na Jari Litmanen, mara 8, na Kipa wa Czech Republic Petr Cech mara 8.

Lakini hao wote wamestaafu Timu za Taifa wakati Mkhitaryan bado anacheza akikimbizwa kwa karibu na wale ambao bado wanadunda Timu zao za Taifa kina Gareth Bale wa Wales na David Alaba wa Austria, wote wakiwa na Tuzo 6 kila mmoja.

Wengine waliowahi kutwaa Tuzo 6 enzi zao ni Andriy Shevchenko wa Ukraine na Aliaksandr Hleb wa Belarus.

Walotwaa mara 5 ni Marek Hamsik (Slovenia), Robert Lewandowski (Poland), Goran Pandev (Macedonia) na Mstaafu Kakha Kaladze (Georgia).

Kwenye baadhi ya Nchi Tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka zina mifumo tofauti kama vile Portugal ambako zipo za aina mbili za yule achezae Ligi ya ndani na yule achezae nje ya Nchi.

Huko, kwa Wachezaji wa nje, Cristiano Ronaldo amezoa mara 8 katika Miaka 10 iliyopita.

Na Argentina wana mfumo wa aina hiyo hiyo ingawa kabla haijabaguliwa Lionel Messi alibeba Tuzo mara 2 na ilipotofautishwa kati ya Wachezaji wa ndani na nje, Messi alipewa mara 8 kati ya 9 kwa wa nje tangu wakati huo.


Straika wa Mabingwa wa England Leicester City anaechezea England Jamie Vardy sasa atakosa Mechi 3 baada ya Rufaa yake kupinga Kadi Nyekundu aliyopewa Jumamosi Leicester ikitoka 2-2 na Stoke City kutupiliwa mbali.

Vardy, mwenye Miaka 29, atazikosa Mechi za Leicester dhidi ya Everton, West Ham na Middlesbrough.

Vardy alitolewa nje na Refa Craig Pawson katika Dakika ya 28 kwa Rafu ya Miguu Miwili kwa Straika wa Stoke Mame Diouf.


KILE Kifungo cha Real Madrid walichoshushiwa na FIFA cha kutosajili Wachezaji Wapya hadi Januari 2018 sasa kimepunguzwa na CAS, Court of Arbitration for Sport, Mahakama ya Usuluhishi Michezoni, na sasa wataruhusiwa kusajili Wapya kuanzia Julai, 2017.
Awali FIFA iliwafungia Real kutosajili Wachezaji Wapya kwa Madirisha Mawili ya Uhamisho ikimaanisha yale ya Januari 2017 na Julai 2017 kwa kosa la kusajili Wachezaji wa chini ya Miaka 18 kinyume na Kanuni za FIFA,
Vile vile, CAS imeipunguza Faini waliyotozwa Real kutoka Pauni 282,000 hadi Pauni 188,000.
Adhabu hiyo ya FIFA walipewa Real na pia wenzao wa Jiji la Madrid Atletico Madrid Mwezi Januari lakini Klabu hizo zilikata Rufaa na hivyo kupata mwanya wa Kusajili mwanzoni mwa Msimu Mwezi Julai.
Hata hivyo, FIFA ikazitupa Rufaa za Klabu hizo mbili na zote zikaamua kukata Rufaa kwa CAS.
Kupunguziwa Adhabu kwa Real kumetobolewa kupitia Tovuti ya Klabu hiyo lakini hamna habari yeyote kuhusu maamuzi ya CAS kwa Rufaa ya Atletico Madrid.



Miss Puerto Rico Stephanie Del Valle is crowned after winning the Miss World 2016 Competition in Oxen Hill, Maryland, U.S., December 18, 2016. REUTERS/Joshua Roberts
Miss Puerto Rico Stephanie Del Valle (C) reacts to being named Miss World as Miss Philippines Catriona Elisa Gray (L) and Miss Kenya Evelyn Njambi Thungu watch during the Miss World 2016 Competition in Oxen Hill, Maryland, U.S., December 18, 2016. REUTERS/Joshua Roberts
Winner of Miss World Miss Puerto Rico Stephanie Del Valle (C) stands with first runner up Miss Dominican Republic Yaritza Miguelina Reyes Ramirez (L) and second runner up Miss Indonesia Natasha Mannuela during the Miss World 2016 Competition in Oxen Hill, Maryland, U.S., December 18, 2016. REUTERS/Joshua Roberts
Winner of Miss World Miss Puerto Rico Stephanie Del Valle (C) stands with first runner up Miss Dominican Republic Yaritza Miguelina Reyes Ramirez (L) and second runner up Miss Indonesia Natasha Mannuela during the Miss World 2016 Competition in Oxen Hill, Maryland, U.S., December 18, 2016. REUTERS/Joshua Roberts
Miss Puerto Rico Stephanie Del Valle reacts after winning the Miss World 2016 Competition in Oxen Hill, Maryland, U.S., December 18, 2016. REUTERS/Joshua Roberts


RATIBA LIGI  KUU ENGLAND
Ijumaa Desemba 23

African Lyon v Yanga [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]
 

Jumamosi Desemba 24
Mbeya City v Toto Africans [Sokoine, Mbeya]
Kagera Sugar v Stand United [Kaitaba, Bukoba]
Ndanda FC v Mtibwa Sugar [Nangwanda, Mtwara]
Simba v JKT Ruvu [Uhuru Stadium, Dar es Salaam]
Majimaji FC v Azam FC [Majimaji, Songea]
Mwadui FC v Mbao FC [Mwadui Complex, Mwadui]

Jumatatu Desemba 26

Ruvu Shooting v Tanzania Prisons [Mabatini, Mlandazi]


RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND BOXING DAY
Jumatatu Desemba 26
15:30 Watford v Crystal Palace
18:00 Arsenal v West Bromwich Albion
18:00 Burnley v Middlesbrough
18:00 Chelsea v Bournemouth
18:00 Leicester City v Everton
18:00 Manchester United v Sunderland
18:00 Swansea City v West Ham United
20:15 Hull City v Manchester City

Jumanne Desemba 27
20:15 Liverpool v Stoke City

Jumatano Desemba 28
22:45 Southampton v Tottenham Hotspur

Ijumaa Desemba 30

2300 Hull City v Everton

Jumamosi Desemba 31
1800 Burnley v Sunderland
1800 Chelsea v Stoke City
1800 Leicester City v West Ham United
1800 Manchester United v Middlesbrough
1800 Southampton v West Bromwich Albion
1800 Swansea City v Bournemouth
2030 Liverpool v Manchester City

Jumapili Januari 1

16:30 Watford v Tottenham Hotspur
19:00 Arsenal v Crystal Palace

Jumatatu Januari 2
1530 Middlesbrough v Leicester City
1800 Everton v Southampton
1800 Manchester City v Burnley
1800 Sunderland v Liverpool
1800 West Bromwich Albion v Hull City
2015 West Ham United v Manchester United

Jumanne Januari 3
22:45 Bournemouth v Arsenal
23:00 Crystal Palace v Swansea City
23:00 Stoke City v Watford 20:00

Jumatano Januari 4
2300 Tottenham Hotspur v Chelsea

Wednesday, December 14, 2016


MCHEZAJI wa Kimataifa wa Algeria Riyad Mahrez ametwaa Tuzo ya BBC ya Mchezaji Bora Afrika kwa Mwaka 2016.
Mahrez, Mzaliwa wa France mwenye Miaka 25, aliisaidia mno Leicester City kutwaa Ubingwa wa England Mwezi Mei kwa mara ya kwanza katika Historia yao na hilo limempa Tuzo hii maarufu na inayosifika ya BBC, Shirika la Utangazaji la Uingereza.
Mapema Mwaja huu, Mahrez alitunukiwa Tuzo ya PFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka kwa England baada ya kuifungia Bao 17 na kutoa Msaada wa Bao 11 kwenye EPL, Ligi Kuu England, na kuwa Mchezaji wa Kwanza kutoka Afrika kuwahi kushinda Tuzo hiyo ya PFA, Professional Footballers Association, ambacho ni Chama cha Kutetea Maslahi ya Wanasoka wa Kulipwa.

Mahrez alishinda Tuzo hii ya BBC kwa kuzoa Kura nyingi za Mashabiki na kuwabwaga Wagombea wengine ambao ni Yaya Toure, Sadio Mane, Pierre-Emerick Aubameyang na Andre Ayew.
Mahrez, ambae alijiunga Leicester Mwaka 2014 akitokea Klabu ya France Le Havre kwa Dau la Pauni 400,000, sasa anaungana na kina Didier Drogba na Staa wa Liberia George Weah ambao waliwahi kushinda Tuzo hii.


CRISTIANO RONALDO ameshinda Tuzo maarufu na iliyotukuka ya Ballon d'Or kutoka Listi ya Wagombea 30 akiwemo alieishika kmWaka Jana Lionel Messi. Cristiano Ronaldo lifts the European ChampionshipHii sasa ni mara ya 4 kwa Ronaldo kutwaa Tuzo hii akizidiwa mara 1 tu na Messi.
Ballon d'Or inasimamiwa na Jarida maarufu France Football na Mshindi wake hupatikana kwa Kura za Wanahabari 173 toka kila pembe ya Dunia.
France Football imekuwa ikisimamia Ballon d'Or kila Mwaka tangu 1956 lakini kwa Miaka 6 iliyopita wamekuwa wakishirikiana na FIFA na Tuzo ya Mchezaji Bora Duniani wa Mwaka kuitwa FIFA Ballon d'Or
Lakini Mwezi Septemba FIFA ikajitoa na kuanzisha Tuzo yao ikuwemo zile za Kinamama, Timu ya Mwaka na Washindi wake wanategemewa kutangazwa kwenye Hafla maalum hapo Januari 9 huko Zurich.
Ronaldo, ambae amefunga Bao 48 katika Mechi 52 kwa Klabu yake Real Madrid na Nchi yake Portugal kwa Mwaka huu 2016, hakuwepo huko France kuipokea Tuzo hiyo kwa vile yuko Japan na Real ambao watashiriki Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.
Mwaka huu, Ronaldo aliisaidia Real kutwaa Ubingwa wa Ulaya na pia Portugal kubeba EURO 2016, Kombe la Mataifa ya Ulaya.
Ronaldo, ambae pia ametwaa Ballon d'Or katika Miaka ya 2008, 2013 na 2014, ameeleza: “Kwangu mimi hii ni heshima kubwa kutwaa huu Mpira wa Dhahabu kwa mara ya 4. Ni ndoto iliyotimia. Nimefurahi sana! Nawashukuru Wachezaji wenzangu, toka Timu ya Taifa na Real Madrid. Basikia fahari na furaha kubwa!”

RONALDO katika Namba:

4 – Ushindi Ballon d'Or Miaka ya 2008, 2013, 2014 na 2016 akiteuliwa mara 8 kugombea.
137 – Mechi kwa Portugal.
68 – Goli kwa Portugal.
4 – Mwaka huu amekuwa Mchezaji wa Kwanza kufunga katika Fainali za EURO (2004, 2008, 2012 na 2016).
80 – Pauni Milioni walizolipa Real Madrid kumnunua kutoka Manchester United 2009.
17 – Rekodi ya Bao nyingi kwa Msimu Mmoja wa UEFA CHAMPIONS LIGI (2014).
270 – Idadi ya Magoli kwa Real Madrid katika Mechi 248 za La Liga.
9 – Jumla ya Mabao kwenye EURO akifungana na Michel Platini kuwa Wafungaji Bora wa Mashindano hayo ya Mataifa ya Ulaya.
14.1 – Pauni anazovuna kutoka kwa Udhamini wa Nike.
48,756,584 – Wafuasi Mtandao wa Twitter.
118,164,346 – Wafuasi Mtandao wa Facebook

WAGOMBEA 30 WA 2016 Ballon d'Or:

Sergio Aguero (Manchester City), Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund), Gareth Bale (Real Madrid), Gianluigi Buffon (Juventus), Cristiano Ronaldo (Real Madrid), Kevin de Bruyne (Manchester City), Paulo Dybala (Juventus), Diego Godin (Atletico Madrid), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Gonzalo Higuain (Juventus), Zlatan Ibrahimovic (Manchester United), Andres Iniesta (Barcelona), Koke (Atletico Madrid), Toni Kroos (Real Madrid), Robert Lewandowski (Bayern Munich), Hugo Lloris (Tottenham Hotspur), Riyad Mahrez (Leicester City), Lionel Messi (Barcelona), Luka Modric (Real Madrid), Thomas Muller (Bayern Munich), Manuel Neuer (Bayern Munich), Neymar (Barcelona), Dimitri Payet (West Ham), Pepe (Real Madrid), Paul Pogba (Manchester United), Rui Patricio (Sporting Lisbon), Sergio Ramos (Real Madrid), Luis Suarez (Barcelona), Jamie Vardy (Leicester City), Arturo Vidal (Bayern Munich).


DROO ya Raundi ya Mtoano ya UEFA CHAMPIONS LIGI imefanyika huko Nyon, Uswisi na Mabingwa Watetezi Real Madrid kupangwa kucheza na Napoli.
Arsenal ya England itacheza na Vigogo wa Germany wakati PSG ikiivaa FC Barcelona.
Manchester Citi itaikwaa Monaco wakati Mabingwa wa England Leicester City wakicheza na Sevilla ya Spain.
DROO KAMILI:
Sevilla v Leicester
PSG v Barcelona
Leverkusen v Atletico Madrid
Porto v Juventus
Bayern Munich v Arsenal
Benfica v Borussia Dortmund
Real Madrid v Napoli
Manchester City v Monaco
Mechi za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 za UCL zitachezwa Tarehe 14/15 na 21/22 Februari na Marudiano ni Tarehe 7/8 na 14/15 Machi.

TAREHE MUHIMU:MECHI ZA MTOANO:
14/15 na 21/22 Feb 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Kwanza
7/8 na 14/15 Machi 2017: Raundi ya Mtoano ya Timu 16, Mechi ya Pili
11–12/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Kwanza
18–19/04/17: Robo Fainali, Mechi ya Pili
02–03/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Kwanza
09–10/05/17: Nusu Fainali, Mechi ya Pili
03/06/17: Fainali (National Stadium of Wales, Cardiff)


Leo Jumatano zipo Mechi 8 za EPL na Vinara Chelsea wapo Ugenini Stadium of Light kucheza na Sunderland, Liverpool Ugenini na Boro, Man United Ugenini na Crystal Palace wakati Spurs wako kwao kucheza na Hull City.
Mechi hizo ni mwendelezo wa Mechi 2 za Jana za Raundi ya 16 ya EPL ambapo Arsenal walipoteza nafasi ya kutwaa uongozi wa Ligi walipotandikwa na Everton 2-1 huko Goodison Park Jijini Liverpool.
Matokeo haya yabaibakisha Chelsea kileleni hata kama Leo watafungwa kwani wana Pointi 37 wakifuata Arsenal wenye 31 na wa 3 ni Liverpool wenye Pointi 31zikifuata Man City 30, Spurs 27 na Man United 24.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumatano Desemba 14

2245 Middlesbrough v Liverpool
2245 Sunderland v Chelsea
2240 West Ham United v Burnley
2300 Crystal Palace v Manchester United
2300 Manchester City v Watford
2300 Stoke City v Southampton
2300 Tottenham Hotspur v Hull City
2300 West Bromwich Albion v Swansea City
 

Jumamosi Desemba 17
1530 Crystal Palace v Chelsea
1800 Middlesbrough v Swansea City
1800 Stoke City v Leicester City
1800 Sunderland v Watford
1800 West Ham United v Hull City
2030 West Bromwich Albion v Manchester United

Jumapili Desemba 18

1630 Bournemouth v Southampton
1900 Manchester City v Arsenal
1900 Tottenham Hotspur v Burnley

Jumatatu Desemba 19
2300 Everton v Liverpool

Sunday, December 11, 2016




Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwapongeza Wasanii mbalimbali waliojinyakulia tuzo zao usiku wa leo,zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar,ambapo Msanii wa muziki wa kizazi kipya Ali Kiba ameibuka kinara kwa kujinyakulia tuzo tatu.

Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akiwa katika picha ya pamoja na Wasanii mbalimbali waliojinyakulia tuzo zao usiku wa leo.

Waziri wa Habari, Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akikabidhi Tuzo ya Heshima kwa DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love baada ya kutangazwa mshindi wa heshima katika tuzo za EATV AWARDS 2016 zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.Tuzo hizo zimeandaliwa na kituo cha Televisheni cha EATV cha jijini Dar es salaam kinachorusha matangazo yake katika nchi za Afrika Mashariki.

DJ Boniventura Kilosa aka Bony Love akipongezwa na DJ John Dilinga mara baada ya kupokea tuzo yake ya Heshima katika tuzo zilizoandaliwa na Kituo cha Televisheni cha EATV.

Mwanamuziki Lady Jay Dee akipongezwa na Mme wake baada ya kupokea tuzo yake katika hafla ya utoaji wa tuzo za EATV AWARDS zilizofanyika kwenye ukumbi wa Malimani City jijini Dar es salaam.

Mwanamuziki Ali Kiba akipokea tuzo yake ya ushindi wa Wimbo Bora wa Mwaka kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania ,Nandi Mwiyombela katika Tuzo za Muziki za EATV AWARDS zilizofanyika usiku huu kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.




























waliotembelea blog