Ameposti kwenye Twitter picha hii |
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Theo Walcott amesaini Mkataba mpya wa miaka minne kuendelea kuichezea Arsenal.
Katika Mkataba huo mpya, Walacott anaingia kwenye orodha ya wachezaji wanaolipwa zaidi kwenye klabu hiyo.
Mpachika
mabao huyo wa England sasa atakuwa anaingiziwa kwenye akaunti yake
benki Pauni 140,000 kila wiki sambambaa na nyota wengine wa The Gunners
akina Alexis Sanchez na Mesut Ozil.
Walcott,
ambaye ndiye mchezaji wa muda mrefu zaidi Arsenal alikuwa anasumbuliwa
na majeruhi msimu uliopita, lakini kwa sasa yuko fiti na alifunga bao
pekee la ushindi dhidi ya Wolfsburg wikiendi iliyopita katika Kombe la
Emirates.
0 maoni:
Post a Comment