Friday, June 5, 2015


James Milner wa Man City ajiunga na Liverpool.
Liverpool wameafikiana Dili ya kumsaini Kiungo wa England James Milner ambae anachezea Manchester City kwa Uhamisho wa bure.
Milner, mwenye Miaka 29, ameshakubaliana malupulupu yake binafsi na Liverpool na atajiunga rasmi nao kama Mchezaji Huru wakati Mkataba wake na City utakapomalizika hapo Julai Mosi kama akifuzu upimwaji Afya yake.
Akiwa na City kwa Miaka Mitano, Milner alifanikiwa kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 2, FA CUP na Kombe la Ligi, Capital One Cup.

Milner pia ameichezea England mara 53.
Msimu uliopita, Milner alianza Mechi 24 na kufunga Bao 8 na kuifungia City Bao 8.
Mchezaji huyu alijiunga na City iliyokuwa chini ya Roberto Mancini Mwaka 2010 kwa Dau la Pauni Milioni 26 akitokea Aston Villa na kuichezea Klabu hiyo jumla ya Mechi 125 na kufunga Bao 18.
Klabu nyingine alizowahi kuzichezea ni Newcastle United na Klabu ya Mji wa Nyumbani kwao Leeds United ambayo alianza kucheza Ligi Kuu England kwa mara ya kwanza Mwaka 2002 akiwa na Miaka 16 tu.

Ilkay Gundogan kujiunga na Manchester United msimu wa 2015/16? Klabu kama Barca, AC Milan na Bayern Munich zilikuwa zikihitaji sahihi yake huku mapema tetesi zikisema wenda akapimwa afya kujiunga na Barcelona.Man United 'set to announce £19.5m transfer, terms already agreed'Ilkay Gundogan Christian Funchs wa Schalke atua Leicester CityMemphis Depay wa PSV - Ni wa Manchester United mpaka sasa akitokea PSV EindhovenMorgan Schneiderlin kujiunga na Klabu ya Man United baada ya kushinda mbio hizo huku Klabu ya Arsenal nayo ikiwa kwenye mchakato huo huo wa kumwania mchezaji huyo.Christian Atsu  wa Chelsea atua kwa Mkopo BournemouthPhilipp - Bayer Leverkusen kwenda Stoke Xavi - Al -SaddKipa Artul Borus - Southampton kwenda BournemouthGraham Dorrans - West Brom kwenda NorwichJoshua King - Blackburn kwenda BournemouthWinger wa Benfica Nicolas Gaitan nae inasemekana kujiunga na Man United
Boyata wa Man City kwenda CelticLuiz Gustavo anukia Old Trafford

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog