Arsenal Leo hii huko Stade Louis II Jijini Monaco Nchini France wana kibarua kigumu cha kupindua historia kwa kufuta kipigo cha Bao 3-1 cha Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu ya UEFA CHAMPIONS LIGI walichopewa na AS Monaco ili kufuzu kucheza Robo Fainali.
Katika historia ya Mashindano haya, hakuna Timu iliyomudu kufuta kipigo cha tofauti ya Bao 2 walichopewa katika Mechi ya Kwanza Nyumbani kwao na kufuzu katika Mechi ya Pili ya Ugenini.
Mbali ya hilo, Arsenal hii Leo wanaivaa AS Monaco, chini ya Kocha makini Leonardo Jardim, ambayo haijafungwa Uwanja wa kwao Stade Louis II kwenye Mechi za Ulaya tangu 2005.
Pia, AS Monaco wana Difensi kigaga ambayo imeruhusu Bao 7 tu katika Mechi zao 22 zilizopita.
Mbali ya vikwazo vyote hivyo, Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal aliewahi kuifundisha AS Monaco, anajiamini kuwa Timu yake itashinda na kufuzu.
Jumatano Barcelona wanaikaribisha Man City huko Nou Camp huku Barca wakiwa mbele kwao 2-1 walizopata huko Etihad.
Nao Borussia Dortmund wako kwao Signal Iduna Park Jijini Dortmund kujaribu kuwatoa Mabingwa Italy Juventus walioshinda 2-1 katika Mechi ya kwanza.
Theo Walcott na Alexis Sanchez kwenye mazoezi
Danny Welbeck
Giroud na Hector
UEFA CHAMPIONS LEAGUE
RATIBA
Marudiano - Raundi ya Mtoano ya Timu 16
Mechi zote kuanza Saa 4 Dak 45 Usiku
Jumanne Machi 17
AS Monaco v Arsenal [3-1]
Atlético Madrid V Bayer Leverkusen [0-1]
Jumatano Machi 18
FC Barcelona v Man City [2-1]
Borussia Dortmund v Juventus [1-2]
0 maoni:
Post a Comment