Msanii
Tekno Miles (wa kwanza kushoto) akizungumza na waandishi wa habari
(hawapo pichani) wakati wa hafla iliyomtambulisha rasmi kwa waandishi wa
habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown
and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon
uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo
pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea
kuanzishwa kwake.
Dj rasmi
wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young Guru” akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla iliyofanyika katika
hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ya kumtambulisha rasmi Msanii
Tekno Miles (Katikati) ambaye anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la
mwisho la “Grown and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika
ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha
wa mwaka mpya. Dj huyo atasimamia vilivyo kazi yake katika shughuli
nzima ya Tamasha hilo.
Meneja
Chapa (pombe kali) wa Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) Shomari Shija
(Kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Msanii Tekno Miles (wa kwanza
kushoto) na Dj rasmi wa msanii Jay Z wa Marekani al maarufu kama “Young
Guru” wakati wa hafla iliyomtambulisha Msanii Tekno Miles kwa waandishi
wa habari iliyofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Msanii huyo anatarajiwa kuburudisha katika Tamasha la mwisho la “Grown
and Sexy, the Gold finale” litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon
uliopo Namanga karibu na Best Bite katika mkesha wa mwaka mpya ambapo
pia atafunga rasmi mfululizo wa matamasha hayo ya Grown And Sexy tokea
kuanzishwa kwake.
Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia kwa umakini mkutano wa
kumtambulisha Msanii maarufu Tekno Miles kutoka Nigeria uliofanyika
katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambaye anatarajiwa
kutumbuiza katika mkesha wa Tamasha la Grown and Sexy the Gold finale
litakalofanyika katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga karibu na
Best Bite jijini Dar es salaam.
Maandalizi
ya Tamasha maarufu la Johnnie Walker “Grown and Sexy The Gold finale”
kwa ajili ya kuuaga mwaka na kuukaribisha mwaka mpya yanaendelea vizuri
ambapo kwa mujibu wa waandaaji wa Tamasha hilo, “Capital events” kupitia
wadhamini wao “Johnnie Walker” chapa maarufu ya pombe kali
inayosambazwa na Kampuni ya bia ya Serengeti wamemleta Msanii Tekno
Miles kutoka Nigeria kutumbuiza laivu katika Tamasha hilo ambalo litakua
la mwisho kabisa katika historia ya matamasha ya Grown and Sexy nchini
Tanzania.
Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika
katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam,Meneja chapa wa pombe kali
SBL Shomari Shija alisema, “Tumeamua kulidhamini Tamasha hili kama njia
mojawapo ya kujumuika na kufurahi kwa pamoja na wateja wetu wa chapa za
Johnnie Walker katika kuuaga rasmi mwaka huu wa 2015.
Bw. Shija aliongeza kuwa katika Tamasha la mwaka huu ambalo ni la
mwisho katika historia ya mfululizo wa matamasha ya Grown and Sexy
waliona ni vema kumleta msanii maarufu toka Nigeria “Tekno Miles” ambaye
aliwasili jana usiku mida ya saa nane akitokea Nigeria tayari kwa
kulipamba Tamasha hilo. Msanii huyo ambaye anatamba na vibao mbalimbali
kwenye anga ya muziki hivi sasa kama Shoki, Duro na Wash atatumbuiza
laivu kwenye Tamasha hilo ambalo litafanyika siku ya mkesha wa mwaka
mpya katika ukumbi wa King Solomon uliopo Namanga, Msasani karibu na
Best Bite.
Sambamba na uwepo wa msanii huyo wengine wataopamba Tamasha hilo
ni Dj Maarufu “Young Guru” ambaye ni Dj rasmi wa msanii Jay Z toka
Marekani ambaye ataisimamia shoo hiyo vilivyo pamoja na malkia wa uswazi
mwanadada “Shaa” kisura wa Tamasha hilo ambaye atasherehesha shughuli
nzima katika usiku wa tukio.
Kwa upande wake Msanii Tekno alisema anafurahia kusherekea mkesha
wa mwaka mpya akiwa Tanzania na kuahidi kuporomosha burudani ya nguvu
kwa mashabiki wake watakaojitokeza kushuhudia Tamasha hilo la kufunga
mwaka.
Naye
Mwakilishi wa Capital events waandaaji wa Tamasha hilo Bw. Justin
Massawe alisema “Tunawakaribisha wapenzi wote wa burudani na chapa ya
Johnnie Walker kujitokeza kwa wingi kushuhudia Tamasha letu la mwisho la
Grown & Sexy na kuahidi kuwa litakuwa la kufana zaidi kwani
wamejipanga kutoa burudani ya nguvu na kuwafurahisha mashabiki
mbalimbali.
“Ningependa kuwashukuru wadhamini wetu mbalimbali katika kipindi
chote cha mfululizo wa matamasha haya tokea yalipoanzishwa rasmi kwa
ushirikiano mzuri ambao wametupatia hadi hii leo tunapofunga rasmi
tamasha hili la mwisho la Grown and Sexy the Gold finale.”
Bw. Justin hakusita pia kuwashukuru Johnnie Walker kwa kuhakikisha
wanakamilisha mikataba yote ya kumleta msanii Tekno Miles pamoja na Dj
Young Guru hapa nchini na kwa kuhakikisha kwamba tamasha la mwisho
linakamilika kwa mafanikio” makubwa zaidi.