JUMAMOSI KESHO HAPATOSHI!! ARSENAL v MAN UNITED - VAN GAAL ATAJA KIKOSI CHAKE CHA KUIUA GUNNERS EMIRATES!! KIPA DE GEA NDANI!
Akiongea huko Aon Training Complex, Carrington Jijini Manchester, Van Gaal alitoboa kuwa Angel Di Maria, David De Gea na Michael Carrick wako fiti kuivaa Arsenal.
Kuhusu kuumia kwa Kiungo Daley Blind ambae alipata tatizo la Goti akiichezea Nchi yake Netherlands, Van Gaal amesema amewekewa sapoti kwenye Goti na atapimwa baada ya Siku 10 lakini hayupo katika hali mbaya kama ilivyofikiriwa.
Arsenal wataingia kwenye Mechi hii ya Jumamosi wakiwa Nafasi ya 6 Pointi 1 tu mbele ya Man United ambayo iko Nafasi ya 7.
Mara ya mwisho Arsenal kuifunga Man United ni Mei Mosi Mwaka 2011 Bao 1-0 Uwanjani Emirates kwenye Mechi ya Ligi na tangu wakati huo wamecheza Mechi 6 na kutoka Sare 2 tu na zote zilizobaki Man United kushinda ukiwemo ushindi wa kishindo wa Bao 8-2 hapo Tarehe 28 Agosti 2012.Van Gaal akiteta jambo na Vijana wake leo IjumaaWachezaji wa United wakijifua leo tayari kwa mchezo wao na Arsenal Emirates.Kazi ipo kesho!Van Gaal na msaidizi wake GiggsNi sisi na Arsenal kesho!
0 maoni:
Post a Comment