Manchester United wameshinda Mechi yao ya kwanza Msimu huu kwenye Ligi Kuu England wakati Kikosi chao kipya kikiisambaratisha QPR kwa Bao 4-0 ndani ya Old Trafford huku Angel De Maria aking’ara na Wachezaji wapya Marcos Rojo na Daley Blind wakicheza Mechi yao ya kwanza na kuleta uhai mkubwa.Juan Mata akifanya yake..
Bao 3 kabla ya Mapumziko, zilizofungwa na Di Maria, Ander Herrera na Wayne Rooney ziliwaua QPR na kuwamaliza kabisa pale Kipindi cha Pili Juan Mata alipofunga Bao la 4.Radamel Falcao akikimbiza mpira mwishoni kipindi cha pili..Radamel Falcao chupuchupu afunge! Kipa wa QPR aliutema mpira..
Straika mpya, Radamel Falcao, alikuwa Benchi na kuingizwa Dakika ya 67 na alionyesha matumaini na nusura afunge Bao kama si uhodari wa Kipa wa Robert Green. Bao la nne lilifungwa na Juan Mata katika dakika ya 58 kipindi cha pili baada ya kupata pasi kutoka kwa Ángel Di María.Ander Herrera akishangilia bao lake la pili kwa United.Angel Di Maria alifunga Bao la Kwanza kwa frikiki murua na ni yeye alietengeneza Bao la Pili kwa kukokota ngoma Mita 60 na kumpasia Rooney aliepiga Shuti lililookolewa na kumrudia Herrera na kufunga.Dakika ya 24 Di Maria anaipachikia bao la kwanza Manchester United..1-0 dhidi ya QPR. Ni Frii kiki ya Di Maria ya umbali wa yadi 30 na kutinga moja kwa moja hadi langoni mwa QPR.Ander Herrera alitupia la pili na kufanya 2-0 dhidi ya QPR katika dakika ya 36 kipindi cha kwanza baada ya kupata mpira kutoka kwa Wayne Rooney. Bao la tatu lilifungwa na Wayne Rooney katika dakika ya 44 kwa shuti kali lililomzidi kipa wa QPR Green na kuzama langoni moja kwa moja na ni kwa ushirikiano wa Ander Herrera aliyetoa pasi kwa Rooney.Falcao alichukua nafasi ya Juani Mata kipindi cja pili dakika ya 67Rojo kwenye patashika na Matt Philips wa QPRFer wa QPR akichuana na Angel Di MariaRio Ferdinand kwenye wasiwasi kutoka kwa timu yake ya zamani UnitedRadamel Falcao kaanzia benchiRio Ferdinand akipewa zawadi yake mapema kabla ya mtanange..Van Gaal kati..Tayari kwa kipute...
Daley Blind na Radomel Falcao wakiingia Old Trafford...yasemekana Falcao kuingia kipindi cha pili..dhidi ya QPR.Wachezaji wa Man United wakiwa tayari kwa kipute na QPR jioni hii kwenye uwanja wa Old Trafford. United wanatarajia kuchezesha wachezaji wao wapya katika mtanange huu.
Daley Blind na Radomel Falcao wa Manchester United wakiwasili kwenye Uwanja wa Old Trafford, Tayari kwa mtanange huo.
Luke Shawna Ander Herrera wakishuka kwenye basi kuingia Uwanjani Old Trafford.
Meneja wa Man United Louis van Gaal akiwsiliWachezaji wa QPR wakiwa kwenye Uwanja wa Old Trafford
Mashabiki nao ndio kwanza wanaanza kuingia kuchukua nafasi zao Uwanjani Old Trafford.
VIKOSI:
0 maoni:
Post a Comment