Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo.
Basi la Kampuni ya Hood likiwa limepinduka na watu kuumia vibaya eneo la Same leo asubuhiBaadhi ya wasamalia wema wakiwaokoa abiria waliokuwa wamepanda basi hilo la hood lililokuwa linatoka Arusha kwenda Mbeya baada ya kupinduka.
Ajali
hiyo imetokea katika, barabara ya Same - Mwanga, Kijiji cha Kiverenge
wilaya ya Mwanga mkoani Kilimanjaro ambapo taarifa za awali zinasema kuwa chanzo chake ni kupasuka kwa tairi ya mbele.
Kamanda
wa polisi mkoani Kilimanjaro, Robert amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo ambapo amesema katika ajali hiyo alifariki Abiria mmoja aliyemtaja
kwa jina la Joshua Likumbia, Raia wa Kenya, ambaye alikuwa akisafiri
kuelekea jijini Mbeya.
Kamanda
Boaz amesema majeruhi katika ajali hiyo ambao ni 16, akiwemo dereva wa
Basi, Fadhili Hashim wamelazwa katika Hospitali ya wilaya ya Same na
Hospitali ya Rufaa mkoani Kilimanjaro, KCMC.
0 maoni:
Post a Comment