Tel: 0712461976/0764302956
WEKUNDU
wa msimbazi Simba “Taifa kubwa” wameanza mazoezi katika uwanja wa
Kinesi jijini Dar es salaam chini ya kocha wake mkuu, Mcroatia Dravko
Logarusic, kujiwinda na mtanange wa vuta ni kuvute dhidi ya Maafande wa
Tanzania Prisons “wajelajela” katika dimba la sokoine jijini Mbeya
jumapili machi 9 mwaka huu.
Afisa
habari wa Simba, Asha Muhaji ameuambia mtandao huu kuwa baada ya mechi
ya jumapili dhidi ya Ruvu Shooting waliyoshinda mabao 3-2, waliwapa
mapumziko ya siku moja wachezaji wao ili kujipanga na maandalizi ya
mechi ijayo.
“Sisi
tuna utaratibu wa kuwapumzisha wachezaji wetu kwa siku moja baada ya
mechi, hivyo jumatatu hawakuwa na mazoezi, na hapo jana wameanza mazoezi
kinessi na watakuwa hapo mpaka siku ya safari yetu kuelekea Mbeya”.
Alisema Muhaji.
0 maoni:
Post a Comment