.
Mitambo
Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha Adam Kigoma Malima alifanya ziara ya siku
mbili mkoani Kagera na kukagua miradi ya ujenzi wa vituo vya umoja wa ushuru na forodha (One Stop Border Post)Rusumo na Mtukula na ujenzi wa daraja la Kimataifa la Rusumo kati ya
Tanzania na Rwanda.
Naibu Waziri Adam Malima alifanya ziara hiyo mkoani Kagera kuanzia
tarehe 29 -30 Januari, 2014 na kutembelea mpaka wa Rusumo Wilayani Ngara na
Mtukula Wilayani Missenyi pia kuongea na wananchi na wafanyabiashara na kutatua
kero zao.
Katika mradi wa ujenzi wa Kituo cha pamoja cha ushuru na
forodha Rusumo mpakani mwa Tanzania na
Rwanda Naibu Waziri alikagua ujenzi unavyoendele ikiwa ni pamoja ujenzi wa
daraja la kimataifa la Rusumo ambalo ni la kisasa.
Daraja hilo llitakalokuwa na
urefu wa kilometa 2 na upana wa meta 10.5 linajengwa kwa gharama ya Yeni za
Kijapani blioni 2.9 na kila nchi (Tanzania na Rwanda) zinachangia fedha za
Japani Yeni bilioni 1.4 kila nchi mpaka
daraja kukamilika ujenzi wake.
Kwa upande wa Tanzania mradi wote
(Kituo cha pamoja cha ushuru na forodha na daraja) umefadhiliwa na Serikali ya Japani kwa gharama ya fedha za Japani Yeni bilioni 1.8 na unajengwa na Kampuni ya Kijapani iitwayo DAIHO
COOPERATION abapo ujenzi wake umefikia
asilimia 68.
Baada ya kukagua na kujionea
ujenzi unavyoendelea Naibu Waziri Malima aliwahakikishia wananachi na
wafanyabiashara kuwa serikali itahakikisha mradi huo unatekelezwa na kukamilika
kwa muda uliopangwa ambapo ulianza 2 Machi, 2012 na unatarajia kukamilika 15
Novemba, 2014
Naibu Waziri Malima aliwahakikishia wananchi na
wafanyabiashara katika mpaka huo kuwa mara baada ya ujenzi wa Kituo cha pamoja
cha ushuru na forodha kumilika na daraja la kimataifa kukamilika mpaka wa
Rusumo utaanzan kufanya kazi kwa masaa
24 kutoka 16 ya sasa.
Aidha akisikiliza kero za
wananachi wa Rusumo waliolalamika kuhusu huduma ya maji na umeme katika mpaka
huo, Naibu Waziri Malima alisema ili kituo cha pamoja cha ushuru na
forodha kifanye kazi masaa 24 ni lazima
kuwepo na umeme wa uhakika katika eneo husika
na kufikia muda wa mradi kukabidhiwa kila kitu kinachohitajika kitakuwa
tayari kimetekelezwa na serikali.
Katika Wilaya ya Missenyi Naibu
Waziri wa Fedha Adam Malima alitembelea na kukagua Kituo cha pamoja cha ushuru
na forodha Mtukula kwenye mpaka wa Tanzania na Uganda ambacho kimekamilika
ujenzi wake kwa asilimia 100 na kuanza kutoa huduma..
Kero kubwa iliyokuwa inaleta
kelele nyingi katika mpaka huo ilikuwa ni umeme ambapo Naibu Waziri Malima
alihakikishiwa na Meneja wa TANESCO mkoa wa Kagera Bw. Martin Maduro kuwa
kufikia tarehe 28/02/2014 umeme utakuwa
tayari unawaka katika mpaka huo na mafundi wanaendelea na kazi.
Katika hatua nyingine Naibu
Waziri Malima aliwaagiza Mamlaka ya Mapato nchini kuwajibika kwa uwazi mfano
kutoza ushuru katika bidhaa mbalimbali ili kuondoa malalamiko ya wananchi na wafanyabiashara ambao ndiyo wateja wao au walipa kodi.
Wafanyabiashara wa Mazao
walilalamika kuhusu vibali vya kusafirisha mazao kuwa vinapatikana Wizarani Dar
es Salaam tu jambo ambalo linawafanya kuongeza gharama katika mazao hayo bila
sababu na kumwomba Naibu Waziri Malima kuwa vibali hivyo vipatikane katika Wilaya zao.
Akijibu suala hilo Naibu Waziri
Malima alisema kuwa wizara Fedha
ikishirikiana na Wizara ya Biashara na Viwanda, na Wizara ya Kilimo wataweka
utaratibu mzuri wa kuhakikisha vibali
hivyo vinapatikana kilahisi ili kupunguza gharama na usumbufu kwa wafanyabiashara
mipakani kwa nchi nzima.
Naibu Waziri Malima alimalizia
kwa kuwahawahakikishia wafanyakazi wa mipakani katika idara zote zinazohusika
katika kituo cha pamoja cha ushuru na forodha (One Stop Border Post) kuwa serikali imeanza kutafuta ufumbuzi wa kero ya makazi yao
katika mipaka ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa masaa 24 bila kuhathili
utoaji wa huduma katika mipaka hiyo.