MSANII wa muziki wa asili aliyewahi kutamba na
wimbo wa ‘Maria Salome’ uliokuwa maarufu kwa jina la ‘Chambua Kama
Karanga’, Saida Karoli amesema umaarufu aliokuwa nao haukufanana na kile
alichokitia mfukoni.
Mkali huyo wa Kaisiki na Mapenzi kizunguzungu
alisema alitembea nchi nyingi duniani bila kuingiza kipato kikubwa
mfukoni mwake kutokana na kulipwa mshahara na meneja wake hata kama
angefanya kazi kubwa na shoo zilizoingiza kipato kikubwa.
“Siwezi kuweka wazi mshahara niliolipwa ila
nakumbuka nilifanya shoo za kulipwa kwa dola na kuzunguka nchi
mbalimbali duniani ila nililipwa kwa fedha ya Kitanzania tena mshahara
uleule kila mwezi, nashukuru kwa sasa ninajisimamia mwenyewe ninapata
fedha nyingi sana ingawa sina jina kama zamani,” aliweka wazi Saida
Karoli.
Kwa sasa msanii huyu ameweka makazi yake jijini Mwanza huku akitamba na wimbo wa Mashamsham na albamu yake ya Pesa Inawasha.
0 maoni:
Post a Comment