Saturday, December 21, 2013

HATIMAYE mshambuliaji Emmanuel Okwi amewasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam jioni hii tayari kuanza kuutumikia Mkataba wake wa miaka miwili katika klabu ya Yanga.
Mshabuliaji huyo wa zamani wa Simba alitua kwa ndege ya RwandaAir Saa 9:55 jioni na kulakiwa na viongozi na mamia ya wapenzi kadhaa wa timu ya Yanga kabla ya kupakiwa kwenye gari ndogo alilokuwa akiendesha Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Kimataifa ya Yanga, Seif Ahmed na kuondoka.
Mbali na Ahmed aliyekuwa akiendesha gari Okwi alikaa kiti cha nyuma sambamba na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Mussa Katabaro.
Okwi alitokea geti la wageni maalum na kusindikizwa na Polisi huku, umati wa mashabiki wa Yanga ukimshangilia na kumfanya atoke kwa taabu hadi kupanda gari.

Habari ya Okwi kuhamia Yanga, bado kuna utata -ungependa aidhinishe kuichezea Yanga ama asiidhinishwe?

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog