Mwili wa Marehemu Dk. Sengondo Mvungi ukifanyiwa maombi mara baada ya
kuwasili Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo.
Wanachama wa NCCR-Mageuzi wakiwa wamelibeba sanduku lililohifandhi
mwili wa kiongozi huyo wa NCCR-Mageuzi na Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko
ya Katiba Mpya.
Waombolezaji waliofika uwanjani hapo kuupokea Mwili wa Dk. Mvungi.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akiwa uwanjani hapo.
Baadhi ya waombolezaji waliofika uwanjani hapo.
Mjane wa Marehemu, Bi Anna Mvungi akiwa uwanjani hapo kuupokea mwili wa mumewe
Mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya mabadiliko ya Katiba mpya na Mkurugenzi wa Katiba, Sheria na Haki za Binadamu wa NCCR-Mageuzi, Marehemu Dk. Sengondo Mvungi umewasili nchini kutoka Afrika Kusini.
Makumi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ndugu jamaa na marafiki wa
Marehemu dk. Sengondo Mvungi walifika uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius
Nyerere upande wa Mizigo na kuupokea mwili wa kiongozi huyo na mwana
familia.
Mapokezi ya mwili wa Dk. Mvungi aliyefariki juzi kufuatia majeraha ya
shambulizi la majambazi lililomkuta nyumbani kwake nombemba 2 mwaka huu
na kupeleka Nchini Afrika Kusini kwa Matibabu, yaliongozwa na Mkewe mama
Anne Mvungi.
Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba mpya, Jaji na Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde
Warioba, Waziri wa Uchukuzi, Dk. Sengondo Mvungi, Mwenyekiti wa
NCCR-Magezi, na wajumbe takriban wote wa tume ya mabadiliko ya Katiba
mpya.
Sanduku hilo lilifunikwa bendera ya Chama cha NNCR-Magezi.
Mwili wa marehemu Dk. Sengondo Mvungi unataraji kuagwa kesho katika
viwanja vya Karimjee kabla ya kusafirishwa kwenda kijijini Kwao
Kisangara juu, Wilaya ya mwanga mkoani Kilimanjaro kwa Maziko siku ya
jumatatu.
________________
MUDA
|
TUKIO
|
LEO, NOVEMBA 15, 2013 – UWANJA WA NDEGE WA MWALIMU JK NYERERE
| |
Saa 12:50 jioni
|
Kuwasili kwa mwili wa Marehemu – Uwanja wa Ndege wa Mwalimu JKN
|
KESHO, NOVEMBA 16, 2013 – VIWANJA VYA KARIMJEE
| |
Saa 2:00 – 3:30 asubuhi
|
Kuwasili kwa Wageni, Wananchi na Waombolezaji
|
Saa 3:30 asubuhi
|
Kuwasili Mwili wa Marehemu
|
Saa 4:00 – 5:45 asubuhi
|
Ibada ya Misa Takatifu, Viwanja vya Karimjee
|
Saa 5:45 – 6:55 mchana
|
Salaam za Rambirambi na Neno la Shukurani
|
Saa 6:55 – 8:40 Mchana
|
Kuaga Mwili wa Marehemu
|
Saa 9:00 Alasiri
|
Msafara kupeleka mwili wa marehemu Kibamba Msakuzi
|
KESHO KUTWA, NOVEMBA 17, 2013 – NYUMBANI KWA MAREHEMU – KIBAMBA, MSAKUZI
| |
Saa 2:30 – 4:30 asubuhi
|
Ibada ya Misa nyumbani kwa marehemu
|
Saa 5:00 asubuhi
|
Kuanza safari ya kwenda Chanjale, Kisangara Juu, Mwanga, Kilimanjaro
|
0 maoni:
Post a Comment