Friday, October 25, 2013

Msanii Alaine Laughton (katikati) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa wasanii wa kimataifa watakaotoa burudani katika tamasha la Serengeti Fiesta 2013 leo katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar Es Salaam. Kushoto ni msanii ktoka Nigeria David Adeleke (Davido) na Kulia ni Meneja masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti Allan Chonjo.Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba Akiongea na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa mkutano na wahandishi wa habari leo kwaajili ya kuwatambulisha wasanii watakaofanya makamuzi kwenye stage ya serengeti fiesta 2013 hapo Kesho Jumamosi katika Viwanja vya Leaders.Meneja Masoko wa kampuni ya bia ya Serengeti, Allan Chonjo akiwatambulisha baadhi ya wasanii watakaotoa burudani katika tamasha la Serengeti Fiesta 2013 kutoka nje ya Tanazania, kushoto ni Alaine Laughton kutoka Jamaica na Mohombi Nzasi Moupondo kutoka Sweden. Hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Serena iliyopo katika jiji la Dar ES Salaam.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog