Wednesday, October 23, 2013

Hii stage bado ikiwa haijakamilika ikiwa bado kwenye kutengenezwa (Underconstruction) ni kati stage za kisasa ambayo itaonekana siku hiyo ya Serengeti Fiesta 2013 katika viwanja vya Leaders Club Jumamosi 26 Oktoba 2013 kwa kiingilio cha shilingi 10,000/= Tz kama ukikata tiketi yako mapema na mlangoni utalipa shilingi 15,000/= TZ huku ukipata nafasi ya kuwashuhudia wasanii wakimataifa zaidi ya mmoja ikiwa ni tofauti na Fiesta zote zilizopita, wasanii wakimataifa wannne kwa wakati mmoja hapa namzungumzia Iyanya, Davido, Alaine na Mohombi huku wakipigwa tafu na wasanii wakali kutoka nchini Tanzania. Stage inahitaji siku 10 mpaka kukamilika, kuna vitu vingi vya kustaajabisha kuhusiana na stage hii ni stage tofauti ni kubwa sana ambayo ina njia inayomfanya msanii atembee katikati akiwa amezungukwa na mashabiki kulia na kushoto kwake ndo maana Fiesta ya mwaka 2013 Ni Noma Saana!! Twenzetu — Usikose.
Hii ni nyumba ambayo itakuwa backstage ambayo itakuwa na bar na makochi comfortable ambayo yatatumiwa na watu watakao kuwepo katika eneo hilo wakiwemo wasanii huku wakisubiri kwenda kutoa burudani kwa mashabiki wa Serengeti Fiesta -- Noma Saana!! TWENZETU 

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog