Thursday, September 5, 2013

Wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wametoka nje muda huu baada ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Mhe. Freeman Mbowe kuamriwa atolewe nje na Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai. 


Mbowe alisimama ili achangie lakini aliamriwa na Job Ndugai kukaa chini jambo ambalo hakuliafiki na kuendelea kusimama. Baada ya tukio hilo, Ndugai aliwaamuru askari wa bunge kumtoa nje Kiongozi huyo wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na ndipo mzozo ulipotokea. Hali hiyo ilitokea wakati wa Majadiliano ya Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Mabadiliko ya Katiba wa mwaka 2013. Mbowe aligoma kutolewa nje ya bunge baada ya askari kufika alipokuwa amekaa kwa lengo la kumtoa nje, ndipo ilipotokea sintofahamu na mzozo mkubwa ndani ya bunge hali iliyopelekea wabunge wote wa Chadema kutoka nje. Hali kama hii pia ilitokea jana wakati muswada wa marekebisho ya pili ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ukisomwa na kupelekea wabunge wa vyama vya Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi kutoka nje wakishinikiza muswada huo usisomwe hadi maoni ya wadau kutoka Zanzibar yapatikane.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog