Wakala Pere Guardiola ambaye ni mdogo wa Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola ameziambia klabu za Real Madrid na Arsenal kuwa ofa ya paundi milioni 40 itatosha kumtoa mshambuliaji huyo Liverpool .
Pere Guardiola amesema kuwa ana imani kuwa ofa ya paundi milioni 40 haitakutana na pingamizi lolote toka Liverpool na hivyo kufanya kazi ya kumuuza mchezaji huyo (Suarez) kuwa nyepesi .
Klabu ya Arsenal imepeleka ofa mbili za paundi milioni 30 na paundi milioni 35 kwa ajili ya Suarez ambapo Liverpool imezikataa ofa hizo . Klabu hiyo yenye maskani yake huko Anfield haiko tayari kumuuza Suarez kwenda klabu nyingine ya England na inasemekana kuwa inasubiri ofa toka kwa Real Madrid ambayo ni moja ya timu zinazotaka kumsajili Suarez.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay Suarez amesema kuwa anataka kuondoka Liverpool ambapo ametaja kucheza Ligi ya mabingwa na kuandamwa na vyombo vya habari kama sababu za kutaka kuondoka .
0 maoni:
Post a Comment