Friday, September 30, 2016
Saturday, September 24, 2016
11:23 AM
Unknown
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akikatiza katika Mtaa wa Hamugembe mjini Bukoba alipokwenda kuwafariji waathirika wa tetemeko la ardhi liliua watu 17 na kujeruhi wengine 252 hivi karibuni. Picha na Phinias Bashaya
Bukoba. Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa amewasili mjini Bukoba mkoani Kagera kuwafariji waathirika wa tetemeko la ardhi lililoukumba mkoa huo na kuua watu 17 na kujeruhi wengine 253.
Baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Lowassa alilakiwa na mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare na kwenda moja kwa moja katika mitaa ya Hamugembe na Kashai kuwasalimia wananchi.
Akizungumza na wananchi hao, amesema amekwenda kuwafariji na kuwaunga mkono na kwamba anataka haki itendeke kwa waathirika hao. Lowassa aliyeambatana na mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na kada wa chama hicho, Khamis Mgeja amesema atawasilisha msaada aliokwenda nao kwa mkuu wa mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu.MWANANCHI
11:14 AM
Unknown
Kushoto
ni Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akimkabidhi
Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey D.J Mwanri (Kulia)
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe Mhandisi Methew Mtigumwe akisoma Risala wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru
Baadhi ya wakuu wa Wilaya za mkoa wa Tabora wakiulaki mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili Mkoani humo.
11:02 AM
Unknown
Kipa
wa Timu ya Maji Maji ya Songea "Wana Lizombe", Amani Simba akiruka bila
mafanikio wakati akijaribu kuudaka mpira uliopigwa kwa umaridadi mkubwa
na Mshambuliaji wa Simba, Jamal Mnyate na kuiandikia timu hiyo bao la
kuongoza, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii
katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka
kidedea kwa kuicharaza timu ya Maji Maji mabao 4-0.
Mshambuliaji
wa Timu ya Maji Maji, Enyima Darlington akiruka sambamba na Beki wa
Simba kuwania mpira wa juu katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa,
Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu
ya Maji Maji mabao 4-0.
Mshambuliaji
machachari wa Timu ya Simba, Laudit Mavugo akiondoka na mpira baada ya
kumtoka Beki wa Maji Maji, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa,
Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu
ya Maji Maji mabao 4-0.
Mshambuliaji
wa Timu ya Maji Maji, Enyima Darlington akitoa pasi nzuri ya kichwa kwa
Mchezaji Mwenzake, Alex Kondo, katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara
uliopigwa jioni hii katika Uwanja wa Taifa,
Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu
ya Maji Maji mabao 4-0.
Ibrahim
Ajib wa Simba akimpiga chenda maridadi, Luhanga Mapunda wa Maji Maji,
katika Mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa jioni hii katika
Uwanja wa Taifa,
Jijini Dar es salaam. Simba imeweza kuibuka kidedea kwa kuicharaza timu
ya Maji Maji mabao 4-0.
10:59 AM
Unknown
Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akizungumza
na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena Jijini Dar es
salaam leo kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni wapenzi wa timu ya
Simba na wapenzi wa timu ya Yanga yenye lengo la kuchangisha fedha kwa
ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi, lililoukumba Mkoa wa
Kagera hivi karibuni. Mchezo huo utafanyika kesho kwenye Uwanja wa
Taifa, Jijini Dar es salaam. Kabla ya Mchezo huo, kutakuwa na michezo ya
Utangulizi ambapo Timu ya Bunge ya Mchezo wa Pete (Netball) inakutana
na Timu ya TBC huku Mchezo mwingine ukiwa ni ni kati ya Wasanii wa Bongo
Movie na Bongo Fleva. Mh. Ngeleja amewataka Watanzania kutoka maeneo yote nchini kujitokeza kwa wingi ili kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwasaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi Mkoani Kagera.
Mkurugenzi
wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Alex
Nkeyenge akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Hoteli ya
Serena Jijini Dar es salaam leo kuhusu mechi kati ya wabunge ambao ni
wapenzi wa timu ya Simba na wapenzi wa timu ya Yanga yenye lengo la
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi,
lililoukumba Mkoa wa Kagera hivi karibuni. Nkeyenge amewataka wale wote
watakaojitokeza kwenda kuangalia mchezo huo, wanatakiwa kuwa na tiketi
za Kielekroniki ambazo zitaanza kutumika rasmi kuanzia hiyo kesho, Pia
amezungumzia hali ya usalama katika Uwanja huo kuwa itaimarishwa vizuri
kwani Jeshi la Polisi limejipanga vyema kuhakikisha hatuna tukio lolote
la uvunjifu wa amani litakalojitokeza uwanjani hapo.
Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akionyesha
moja ya vikombe vitakavyokabidhiwa kwa timu zitakazoshinda katika
michezo hiyo ya kesho.
Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akipokea
mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 10, kutoka kwa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Mwananchi Communication LTD, Francis Nanai ikiwa ni
sehemu ya Mchango wao katika kufanikisha zoezi hilo.
Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akipokea
mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milioni tano, kutoka kwa Kaimu
Mkurugenzi wa Tathmini ya Uhai Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF),
Baraka Maduhu ikiwa ni sehemu ya Mchango wao katika kufanikisha zoezi
hilo.
Mwenyekiti
wa Timu ya Bunge (Bunge Sports Club), Mhe. William Ngeleja akipokea
mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi Milioni tano, kutoka kwa
mwakilishi wa Kampuni ya Jubilee Insurance.
Mwenyekiti wa Bunge, Mh. Mussa Azzan Zungu akitoa shukrani kwa niaba ya Bunge kwa wale wote waliojitoa kufanikisha zoezi hilo.
WAKATI
tiketi za elekroniki zitaanza kujaribio welo, Makampuni mbali mbali
wamechangia jumla ya Sh milioni 20 kwa ajili ya kudhamini mchezo wa
wabunge mashabiki wa Yanga na wale wa Simba utakaofanyika leo kwenye
uwanja wa Taifa ambapo Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atakuwa mgeni rasmi.
Makampuni
hayo ni Mwananchi Communication iliyotoa Sh milioni 20, mfuko wa bima
ya afya NHIF na Jubilee Insurance ambazo zote zimetoa Sh milioni 5 kila
mmoja.
Akizungumza
na Waandishi wa habari leo, Mwenyekiti wa Klabu ya Michezo ya Bunge
William Ngeleja ambaye pia ni mnazi wa Simba alisema matokeo ya mchezo
wa kesho ni hishara ya matokeo ya mchezo wa Oktoba Mosi.
Nae
Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom ambayo ndiyo iliyopewa jukumu la
kusimamia mfumo huo, Gallus Runyeta amesema kadi hizo zitatolewa bure
katika mchezo wa leo ikiwa ni majaribio na kuangalia dosari ambazo
zitajitokeza kabla ya kuanza kuzitumia rasmi.
Akizungumzia
jinsi ya kuitumia kadi hiyo, Runyeta alisema “Utajisajili kwa kupiga
*150*50# halafu ni lazima uiwekee pesa kwa Airtel au M-Pesa. Kiwango cha
chini cha kuongeza salio ni Sh 1,000….: “ “Unaweza ukanunua mechi moja
kwa kuandika tarehe na mchezo husika au ukachagua baadhi ya mechi au
ukanunua mechi zote za msimu za timu unayoipenda.
“Unapokwenda
kuingia uwanjani, utaweka kadi yako kwenye alama husika na mlango
utafunguka wenyewe. Ukishaangalia mechi uliyoinunua, hauwezi kesho yake
ukaenda kutazama mechi nyingine ambayo hujailipia. Kadi itasoma kwenye
mechi zilizolipiwa tu. Ukiingia uwanjani hauwezi ukatoka halafu ukarudi
kwa tiketi ileile.
Viingilio
vya mchezo huo utakuwa ni shilingi 3000 kwa mzunguko kijani na bluu,
10000 na 15000 kwa viti vya machungwa, VIP A 200,000, VIP B 100,000 na
VIP C ni 50,000 huku kutakuwa na viti 50 vilivyotengwa ambapo kwa
yoyote atakayekaa hapo atalipia 1,000,000.
Katika
mchezo huo mbali na wabunge pia kutakuwa na mechi ya bongo movie na
bongo fleva ambapo kikosi cha bongo movie kitaongozwa na King Majuto, Dr
Cheni, Check Budi, Muhogo Mchungu na Ray Kigosi wakati kwa upande wa
Bongo Fleva kitaongozwa na Rich One, Kalla Pina, Ally Kiba, Stamina, KR
Muller na H baba.
10:51 AM
Unknown
September
23 2016 Msajili wa vyama vya siasa alitoa msimamo na ushauri wake baada
ya kupokea malalamiko na kupitia maelezo ya pande zote kuhusu mgogoro
wa uongozi uliopo kwenye chama cha wananchi CUF.
Baada ya
upembuzi Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Mutungi alitoa mwongozo kuwa
Prof. Lipumba bado ni mwenyekiti halali wa chama hicho aidha baadhi ya
viongozi na wanachama waliokuwa wamesimamishwa na wengine kufukuzwa,
Jaji mutungi amesema ni wanachama halali.
Baada ya
tamko hilo la Jaji Mutungi Leo September 24 2016, baadhi ya wanachama
wamemsindikiza Prof. Lipumba mpaka makao makuu ya chama hicho yaliyopo
buguruni jijini Dar es salaam kwa ajili ya kumkabidhi ofisi kama
mwenyekiti wa halali wa chama hicho.
Baada ya
wanachama kufika eneo zilipo ofisi hizo geti lilikuwa limefungwa na
walinzi hivyo iliwabidi kuruka ili kulifungua kwa ndani na baada ya
kuingia ofisini Prof Lipumba ameyazungumza haya.
10:46 AM
Unknown
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dk Beatrice Byalugaba
kufanya uchunguzi na kubaini madaktari wa hospitali ya wilaya ya Mafia
wanaomiliki maduka ya dawa nje ya hospitali hiyo na kuwachukulia hatua.
Amesema
ameshangazwa kukuta maduka ya dawa yanayomilikiwa na madaktari nje ya hospitali
hiyo kwani tayari Serikali ilishaagiza kuondolewa kwa maduka ya madaktari
karibu na hospitali wanazofanyia kazi.
Waziri
mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Septemba 24, 2016) wakati alipotembelea
hospitali ya wilaya ya Mafia katika siku ya pili ya ziara yake wilayani mafia.
Kuhusu
tatizo la upungufu wa dawa hospitalini hapo amemuagiza Dk. Beatrice kufanya
utafiti wa aina ya magonjwa yanayowasumbua wananchi wa wilaya hiyo ili
wanapoagiza waagize dawa nyingi za kutibu magonjwa hayo.Pia
aliwataka watumishi wa hospitali hiyo wajitahidi kuwahudumia vizuri wagonjwa
licha ya uchache wao. Lengo ni kuhakikisha wanapunguza malalamiko kutoka kwa
wananchi.
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii
(CHF) ili waweze kuwa na uhakika wa kupatiwa matibabu bure kwa kipindi cha
mwaka mzima.
Awali
Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dk. Joseph Mziba alisema mwamko wa wananchi kujiunga
na mfuko wa CHF ni mdogo jambo linalokwamisha upatikanaji wa huduma za afya
wilayani Mafia. Jumla ya wananchi waliojiunga na CHF ni watu 6,000 kati
ya watu 50,000.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Bw. Eric Mapunda ameiomba
Serikali kutoa kibali kwa halmashauri kununua dawa ambazo zinakosekana MSD
kwenye soko moja kwa moja bila ya kupitia utaratibu wa manunuzi.
"Kuna
wakati tunakosa dawa MSD na kulazimika kununua kwa mawakala kwa kufuata
taratibu ya manunuzi. Tunalazimika kununua boksi moja la ambapo boksi moja la panadol
linauzwa sh. 20,000 na tukinunua moja kwa moja sokoni bila ya kufuata utaratibu
huo boksi hilo hilo tunalipata kwa sh. 8,000,”alisema
Baadhi
ya wananchi waliokuwepo hospitalini hapo walieleza malalamiko yao kuhusu lugha
chafu na dharau inayotolewa na baadhi ya madaktari na wauguzi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI, SEPTEMBA 24, 2016
Subscribe to:
Posts (Atom)